Kama wewe ni mtumiaji wa simu na unatumia hizi apps najua utakuwa umekutana na kitu kinakwambia update. Maana yak update ni kama kuboresha au kuongeza kitu kipya kwenye ile apps ya zamani.

Watengenezaji wa apps hizi wanakuwa wameweka mambo mapya ndani ya apps sasa ili uyaone na kuyatumia hayo mambo mapya au muonekano mpya lazima ufanye update ya app yako.

 

Hivi ndivyo ilivyo katika akili zetu. Kunaweza kuwa na fursa nyingi hapo ulipo lakini hutaweza kuziona hadi uongeze uwezo wa akili yako. Hutaweza kuona mambo makubwa yanayokuja kama husomi vitabu.

Mabadiliko yakija yatakuacha kwasababu bado una akili ya zamani. Ili uwezo kupokea mabadiliko makubwa yanayokuja lazima uiandae akili yako kupokea mabadiliko. Lazima uondoe uchafu na vitu ambavyo huvitumii tena uiache akili yako wazi iweze kuingiza mambo mapya.

Kama husomi vitabu maana yake ni kwamba unakuwa haukwendi na wakati. Kuna mambo yatashindwa kutokea kwenye maisha yako kwasababu unatumia akili za zamani. Hakuna kilichoongezeka.

Kama akili zako za mwaka jana ndio hizo hizo unazitumia mwaka huu kamwe usitarajie mambo makubwa ndani yam waka huu. Utapata matokeo sawasawa na ya mwaka jana au matokeo madogo Zaidi ya mwaka jana.

Unataka mambo mapya, unataka Baraka, hakikisha umebadili uwezo wako wa kufikiri. Hakikisha umejiongeza. Hakikisha unaongezeka kila siku. Haya hayawezi kutokea kama unaendelea kupokea vitu vile vile vya kila siku. Yaani wewe hunaga muda wa kusoma vitabu, lakini una muda wa kutazama Tv.

Hujawahi kununua kitabu lakini unanunua magazeti kila siku. Kununua gazeti sio vibaya lakini kama unashindwa kununua vitabu usome utakuwa una matatizo.

Huwezi kujitofautisha na wengine kama husomi vitabu. Huwezi kupata matokeo tofauti na wengine kama akili zako ni sawa na zao. Wakati mwingine unaweza kuweka bidii sana na usione matokeo makubwa kwasababu ufahamu wako ni mdogo. Ukiukuza ufahamu wako hata matokeo utayapata makubwa.

Hakikisha unasoma vitabu Kila siku kama unavyokula na kuoga.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading