HATUA YA 256:  Dunia Inakuhitaji?

jacobmushi
2 Min Read

Ni vyema kujiuliza na kujijibu kama kweli dunia inakuhitaji uendelee kuwepo hapa duniani. Lazima ujiulize hivi siku ukiondoka ni wakina nani wataguswa sana na kifo chako?

Ili ujue ni kwa kiasi gani unahitajika hapa duniani lazima utambue ni thamani gani unatoa kwa dunia. Ni vitu gani vinatoka ndani yako na vinaleta matokeo na mabadiliko hapa duniani?

Kama wewe upo tu hapa kwa ajili ya kustarehe tu ujue kwamba unapoteza maana ya maisha yako hapa duniani. Ni muhimu ukafahamu kwamba kila mmoja ana kusudi lake la kuwepo hapa duniani.

 

Kusudi lako ndio litaifanya dunia iendelee kutamani wewe ubaki na uendelee kuihudumia dunia. Kama bado hadi sasa hujatambua kusudi lako basi bado hujajua kama dunia inakuhitaji kwa kiasi gani.

Ukiondoka duniani ni pengo gani utaacha? Kutokana na kazi yako unayoifanya ni wapi patagusa sana maisha ya wengine kiasi kwamba kutokuwepo kwako maisha yao yapate msukosuko?

 

Lazima ujiulize maswali haya ya muhimu sana ili kutambua thamani yako katika dunia hii. Usije kujikuta unaishi tu bila ya kutambua kwanini upo na thamani gani unatoa kwa ulimwengu huu.

Maisha yako ni jukumu lako, dunia inakuhitaji hasa pale unapokuwa kuna jambo unalitoa ndani yako kwa ajili ya dunia. Pale ambapo unakuwa kuna mabadiliko unayaleta ndani ya dunia. Uwepo wako unaonekana hasa pale unapokuwa kuna jambo unalofanya na linagusa maisha ya wengine.

 

Penda kujiuliza nani atalia siku unakufa? Kwanini watalia? Ni kitu gani wataendelea kukikumbuka kila siku? Chagua kile ambacho unataka watu waendelee kulia na kukumbuka kwa ulichowafanyia.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading