Tatizo sio kwamba huna pesa tatizo ni fikra zako juu ya pesa zilivyo. Unafikiri kwamba siku ukipata pesa utafanya hivi na hivi. Ukweli ni kwamba pesa unazipata kila siku lakini hujui.
Ukibadili unavyofikiri juu ya pesa utakuwa umebadili matatizo yako ya kipesa yote.
“The greatest of evils and the worst of crimes is poverty… our first duty – a duty to which every other
consideration should be sacrificed—is not to be poor.”
George Barnard Shaw
 
Chanzo kikuu cha maovu na uhalifu ni umasikini. Jukum letu la kwanza ambalo kila mmoja anatakiwa awe nalo ni kupambana kabisa kutokuwa maskini. George Barnard Shaw
 
Katika kupambana juu ya kuukimbia umasikini tunatakiwa tuanze kwa kubadili fikra zetu juu ya pesa. Usifikiri kwamba ukiwa na pesa ndio matatizo yako yataisha. Unachotakiwa kuwa nacho sio pesa nyingi maana hata zikiwa nyingi kiasi gani zitakwisha.
 
Unafikiri ni kwanini majambazi huwa hawaachi tabia ya wizi japokuwa wanaweza kuiba pesa nyingi sana?
 
Usipokubali kutengeneza mfumo wa kuingiza kipato kwako utaishia kuwa mtumwa wa pesa. Pesa ndio itakuwa inakusukuma kufanya mambo mbalimbali, utajikuta unafanya chochote ili mradi upate pesa.
 
Soma: KUFIKIRI NA KUTENDA
 
Mimi nakwambia usifanye chochote ili upate pesa fanya kitu sahihi. Tengeneza mfumo sahihi na halali ambao utakuwa unakutengenezea kipato kila wakati. Hii ndio njia ya pekee ya kuukataa umaskini.
 
Wengi ukiwaambia juu ya mfumo hawataki kuelewa. Mtu ataki kufanya kazi kwa nguvu zote kwa miaka michache ili baadae afurahie utajiri miaka yake yote. Mtu anataka apate hela ndogo ndogo za haraka haraka. Akipata hela hizo anatatua matatizo yake yanaishia kisha anarudi tena kutafuta pale matatizo yanapoibuka.
“It is impossible to solve your financial problems with money.” *
Phil Laut
Haiwezekani kutataua matatizo yako ya kipesa kwa pesa. Phil Laut
 
Matatizo yako ya pesa yanajirudia kila siku na hakuna siku utajikuta huhitaji pesa.Hivyo ni muhimu ukubali hili la kutengeneza mfumo ambao utakuletea pesa milele hata kama haupo hai.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading