Kuna michezo kama hukuicheza ukiwa mdogo huku ukubwani itakuja kukusumbua. Hili lina ukweli wake kiasi Fulani japo sio kwa mambo yote.

Tukija kwenye upande wetu wa maisha kuna mambo ambayo unaweza kukutana nayo na ukayaona ni magumu bora uachane nayo. Ukweli ni kwamba huko baadae yatakuja kukusumbua. Kuna sehemu utashindwa kuzifikia kwasababu ya hatua ulizoziruka.

Kuna mambo utashindwa kuyafanya kwasababu ya hatua ulizoziruka kipindi unaanza safari yako ya mafanikio.

Ni muhimu sana ukajua ni mambo yapi ya muhimu ambayo unapaswa kuyashughulikia kabla hujafika mbele ya safari. Kabla hujaingia kwenye mtihani ili uingie ukiwa na uhakika wa kufanya vizuri inakupasa upitie yale maswali ambayo yalikuwa yanakuchanganya kwanza.

Ni kweli huwezi kufanya kila kitu na pia huwezi kujua kila kitu lakini kuna mambo ya muhimu ambayo utayahitaji popote unapokwenda.

Inawezekana ni UJUZI Fulani, unapaswa uwe naoi li uweze kupita kwenye hatua za mbele la sivyo itakubidi uingie gharama kubwa za kuajiri mtu kwa kazi ambayo ungeweza kuifanya mwenyewe.

Inawezekana ni MAARIFA Fulani unapaswa uwe nayo ili yakuwezeshe kupita sehemu zenye vikwazo. Kwasababu hukuyapata wakati huu huko mbeleni utajikuta unalipa gharama kubwa sana ili tu uweze kuendelea mbele.

Inawezekana ni MAHUSIANO kuna sehemu Fulani utashindwa kuvuka sio kwasababu huna vigezo bali ni huna mahusiano mazuri na watu ambao wangeweza kufanyika njia ya wewe kupita kirahisi.

Ni vyema ukakaa chini ukajua ni mambo gani ya muhimu yanapaswa kufanyika sasa hivi ili uweze kuvuka hatua zinazokuja mbele yako za mafanikio.

Inawezekana ni mambo madogo madogo unayoyadharau lakini yakaja kuwa sababu ya wewe kulipia gharama kubwa sana huko baadae.

Mfano wewe unasafiri kwenda nje ya nchi unatakiwa uwe na passport yako, kwa uzembe au kujisahau hukukata passport yako mapema zimebaki siku chache za safari ndipo unagundua huna passport. Gharama ya kawaida ni Tsh elfu 50 na inachukua mwezi mmoja. Lakini kwasababu wewe una haraka ulichelewa umebakiza wiki moja tu unaambiwa ili uipate itakupasa ulipie laki tano. Mtu huyu kama hana hiyo pesa maana yake ni hana safari.

Gharama kubwa imeongezeka na inalipia uzembe ambao uliufanya kwa kujua ama kutokujua. Kuna mambo mengi na gharama nyingi zinaendelea kwenye maisha yetu kumbe tunalipia uzembe wetu wa miaka kadhaa iliyopita.

Usikubali kuendelea kulipia gharama za uzembe miaka ijayo fanya linalopaswa kufanyika kwa wakati.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading