Ukiona mtu anakwambia hana muda au yuko bize sana wala usiumize kichwa sana unatakiwa ujue kwamba huyo mtu hajaamua kulipa lile jambo lako kipaumbele au hajaamua kukupa wewe kipaumbele.

Inawezekana mtu ana majukumu mengi sana ya maisha yake kiasi kwamba anashindwa kufanya mambo mengine ambayo anapaswa kuyafanya kweli lakini pale linapokuja swala la msingi katika maisha yako unapaswa ulitengeee muda wake.

Kipaumbele chako cha kwanza kwenye maisha yako kinatakiwa kiwe mahusiano yako na wale unaowapenda na kuwajali. Hii ni kwasababu baada ya yote unayoyatafuta hao ndio watu watakuwa karibu yako siku zote.

Ukiwa bize na kazi kwasababu tu unamhofu bosi wako ipo siku utakosea na kazi utapoteza utarudi kwa wale ambao ulikuwa unasema huna muda wa kuwa nao karibu.

Ukiwa bize na biashara zako zikifeli ukapata hasara bado utarudi pale nyumbani na watu ambao watakuwa karibu yako tena ni wale ambao unaishi nao kila siku. Anaweza kuwa mume/mke, watoto n.k. hawa ndio wataweza kukufariji na kukutia moyo kuliko watu wengine wowote.

Huwezi kusema unampenda Mungu, una muda na Mungu, Unajali ibada kama watu wa karibu yako huna muda nao na huwafanyii hayo unayosema unamfanyia Mungu. Kama huna muda na mume/mke, au watoto basi hata Mungu utakuwa unamdanganya.

Adamu alipewa bustani, pamoja na mke ambaye ni Hawa alipokosea akaweka kipaumbele bustani akamsahau hawa mwishoe hawa akaingia kwenye mikono ya Nyoka akadanganywa wote wakatumbukia kwenye dhambi.

Haijalishi unatafuta pesa kiasi gani usije kuwaambia hawa watu wa karibu yako huna muda uko bize. Kumbuka yote unayafanya ni kwa ajili maisha yenu yawe bora kama utawasahau utapoteza ubora wa maisha.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading