Yafanya wasiwe na maisha bora na mojawapo ya hayo mambo ni tabia mbaya. Tabia hizi nyingi zimekuwa ni tatizo kwenye maisha ya watu kwani kuziacha imekuwa ni tatizo sana.
Tabia nyingi mbaya huanza kujengeka kidogo kidogo na mwisho wake zinakuwa ni kama ulevi kwenye maisha yetu. Ni hatari sana kama utashindwa kufanya namna kuziacha kwani maisha yako yatakuwa ni gereza kubwa ambalo umejijengea mwenyewe.
Kwanza unapaswa kuanza kutengeneza picha kubwa nzuri ukiona jinsi ambavyo unaishi maisha mazuri bila hiyo tabia inayokutesa. Kama ni kuvuta sigara basi jione ukiwa umeacha ona faida ambazo utakuwa unazipata baada ya kuacha kuvuta sigara. Ona maisha yako yanavyokuwa bora bila ya kuvuta sigara.
Anza mara moja namna ya kuacha tabia hiyo. Tengeneza utaratibu na hatua za kuchukua kila siku ili uache hiyo tabia.
Pili ona mabaya ambayo hiyo tabia umbaya uliyonayo yakitokea kwenye maisha yako. Kama wewe una tabia ya ulevi embu tazama picha ya umaskini ambao ulevi umekuletea, ona magonjwa mabaya yameupata mwili wako kwa kuendekeza tabia hiyo. Ona jinsi ukiteseka kwa kuendeleza tabia hiyo.
Kwa kutengeneza picha hii utaweza sababu za kuacha tabia hiyo na kuanza maisha mapya. Yapo mengi unaweza kuyaona na yakawa sababu ya wewe kuacha tabia hiyo kutokana na tabia yenyewe ilivyo.
Tatu tafuta mtu mmoja unaemwamini anaeweza kukutunzia siri zako kaa nae chini mwelezee tabia hiyo inayokutesa. Mpe kazi ya kukufuatilia kila mara ili kujua kama umeacha tabia yako au lah. Hakikisha mtu huyu nay eye hasumbuliwi na tabia kama yako.
Mtu huyu mpe majukumu ya kukuuliza zile hatua za kuchukua kama umeanza na umefikia wapi. Kwa kumweleza mtu tabia zako na akaamua kukusaidia kuziacha unakuwa umepiga hatua moja kubwa sana ya kwenda kuacha tabia hiyo inayokusumbua.
Endelea mbele usirudi nyuma. Ni safari ngumu sio kitu rahisi sana lakini ukiamua inawezekana kabisa kuacha tabia ambazo zimekuwa ni kero kwenye maisha yako.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”