Katika Maisha vipo vitu vingi tunafanya mara nyingi ni kwa kuiga yale ambayo wengine wanafanya, mengine tunaangalia tangu zamani walikuwa wanafanya na mengine ni asili yetu yaani unafanya kwasababu ndio asili ya kila kiumbe hai.

Shida inakuja kuwa kubwa sana pale unapokuwa unafanya jambo kwasababu watu wengine wanafanya. Hapa ndipo unakuwa unajitengenezea bomu kubwa sana ambalo litakuja kukulipukia mwenyewe baadae.

Kama unachokifanya ni kwasababu watu wengine tena wengi wanafanya basi unakwenda kulipuka muda si mrefu.

 

Ni sawa na madereva magari wapo barabarani kila mmoja na safari zake halafu wakaanza kukimbizana. Kama wewe utakuwa umeona mwenzako anakwenda speed Fulani ukasema ngoja nimfukuzie unaweza jikuta umepitiliza unapokwenda.

Kama usipopitiliza basi unaweza hata kupata ajali. Ni vyema ukajua unapokwenda na ukafuata ramani yako badala ya kukimbizana na matukio ya wengine.

Usifanye vitu kwasababu umeona wengine wanafanya bali fanya kwakuwa kuna kusudi la Mungu unataka kulitimiza. Ukiendeshwa na matokeo unayoona kwa wengine ndipo msukumo wako unakuwa mkubwa utajikuta unafeli kila wakati.

Maisha yako yatakuwa ya ajabu sana kama utakuwa unakwenda kwa kufuata maisha ya wengine wanavyoishi kila wakifanyacho na wewe unataka ufanye.

Lazima kuangalia wengine wanafanya nini hasa wanaofanya kama unachokifanya lakini si vyema kuwaiga tunatakiwa tujifunze kwao.

Unatakiwa uwe na ramani yako ya maisha ambayo wewe na Mungu mnawasiliana na anakupa muongozo vyema na namna ya kuvuka milima na mabonde. Kama utakuwa hauna mawasiliano na Mungu wako utakuwa unakwenda kwa kufuata mkumbo mwisho wa siku unajikuta hakuna mahali ulipofika.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading