Pale inapofika wakati ukaanza kujiona huwezi vitu Fulani kwasababu ya elimu yako ndogo unapoteza uwezo wako mkubwa taratibu.
Kuna maneno ambayo ni hatari sana kujitamkia kwenye Maisha yako kwani yanakuharibu kabisa. Yanakufanya ushindwe kwenye kila jambo unalofanya.
Haya;
Mimi sina Elimu ya Kutosha hivyo hii biashara siiwezi!
Kwetu ni maskini sana hakuna hata mmoja tajiri!
Bado sina uwezo wa kutosha kuanzisha …………….!
Kila Biashara ninayoanza haifiki mbali nina mkosi!
Maneno haya na mengine mengi unayoyafahamu yanaharibu kabisa picha yako ya ndani ya mafanikio. Ukizoea kuyasema haya maneno huwa yanakuja kuwa kweli na hivyo kukurudisha nyuma na kushindwa kufanya mambo ya maendeleo.
Wewe ni mtu mkuu sana na una kitu kikubwa ndani yako. Jitamkie maneno mazuri ambayo yatakujenga na siku moja ufikie ile picha unayoitamani.
Wakati naanza kuandika Makala hizi nilikuwa naogopa nikisema ni nani atanielewa. Lakini nimechukua hatua kidogo kidogo hadi sasa nimefikia na kuandika vitabu. Hivyo usikubali hali yeyote ikurudishe nyuma kwa kujitamkia.
KUMBUKA; Jitamkie maneno mazuri juu yako, jiambie vile unavyotaka kuja kuwa na sio jinsi ulivyo sasa. Anza kujinenea maneno mazuri. Anza kujisemea zile ndoto zako. Sema; mimi ni mshindi, ninazishinda changamoto, ninaendesha gari ya ndoto yangu, Maisha ya wengi yanabadilika kupitia mimi. Mimi ni mtu mkuu sana. Ninainuliwa kutoka mavumbini na kuwa mtu mkuu. Sitaishia kuketishwa na wakuu peke yake bali na mimi ninakuwa mkuu.
Maneno haya yanajijenga ndani ya akili yako na utajikuta unaelekea kwenye mafanikio.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.