Kama ukipata tatizo lolote kwenye maisha yako kuna sehemu ukienda ukajieleza tu unaeleweka na tatizo lako linatatuliwa unaweza kufikiri kwamba upo sehemu nzuri sana. Ukweli ni kwamba upo sehemu ya hatari kuliko nyingine yeyote kwenye maisha yako.

Ni rahisi sana mtu kupenda pale ambapo akipeleka matatizo yake yanatatuliwa. Ni hatari sana kama hayo matatizo ulipaswa kuyatatua mwenyewe lakini anayatatua mtu ambaye unamtegemea.

Ni hatari kwasababu utakuwa unajitengenezea ulemavu wa akili. Kila tatizo unalopata liwe dogo kiasi gani utakuwa unamfikiria yule ambaye anaweza kukusaidia kwa haraka.

Wakati unaendelea kusoma Makala hii endelea kutafakari uone ni sehemu gani hiyo ambayo akili yako huwa inawaza kwenda hasa pale unapopitia magumu. Nikushauri sehemu hiyo kama ni binadamu mwenzako basi anza kuacha kuanzia sasa.

Inawezekana huyo anaekusaidia wala hajui kama anakuaharibu kidogo kidogo. Unajua ni aibu sana mtoto ambaye hakui na baadhi ya mambo ambayo alitakiwa ajifanyie peke yake bado anataka kufanyiwa japo ana umri mkubwa.

Ukiwa katika ufahamu wa aina hii basi unashindwa kufanya chochote. Hata biblia inasema amelaaniwa yeye amtegemeaye Mwanadamu. Mtu wa kwanza ambaye unapaswa kuanza kumfikiria kama msaada wako wakati wa matatizo ni Mungu peke yake.

Mtu wa pili unaepaswa kumfikiria ni wewe. Jitazame wewe mwenyewe kwa vile vitu ulivyonavyo unawezaje kutatua tatizo ulilonalo?

Jitazame kwa uwezo ambao Mungu ameweka ndani yako ni kitu gani unaweza kufanya ili kutatua tatizo lilokujia.

Penda kuipa akili yako majukumu yake ya kutatua matatizo. Akili yako ina uwezo mkubwa wa kufikiri na kukupa suluhisho la yale unayopitia. Unapoweka utegemezi kwa wanadamu wengine unajipa ulemavu wa akili.

Ukiwa mtu wa kutegemea wengine ni ngumu sana watu wengine kuweza kuwa chini yako. Kama wewe mwenyewe unashindwa kujisimamia haiwezekani ukaweza kuwasimamia wengine.

Anza kidogo kidogo kutatua matatizo na kadiri muda unavyokwenda utaona hata matatizo makubwa sana unaweza kuyatatua mwenyewe. Anza sasa jipe majukumu ya maisha yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading