Katika maisha kuna mambo tunafanya kwa kujua ama pasipo kujua na mambo hayo yanakuja kuwa miiba katika safari za mafanikio yetu. Ni vyema sana ukatambua unachokifanya sasa hivi kitaleta madhara gani baadae kwasababu ndiko unapokwenda.

Usijisahau kwa chochote ulichonacho unakafikiri umeshamaliza safari. Waliomaliza safari ni marehemu peke yao. Popote ulipo sasa hivi upo kwenye safari, lolote linaweza kutokea.

Kuwadharau Wengine.

Unaweza kufika sehemu ukaanza kuona watu wengine hawana maana tena kwako. Kama umefika mahali ukawa tayari kuwaumiza wengine ili tu malengo yako Fulani yapite jua kabisa unajitengenezea miiba kwenye safari yako.

Dharau hazipaswi kuwa katika moyo wako wala kiburi kwasababu yote hayo uliyoyapata usingeweza mwenyewe kwa mikono yako. Kuna michango ya watu wengi unaowajua na usiowajua hadi kufika hapo ulipo. Kuna watu wengi wamehusika wewe kufika hatua uliyopo na wengine ulishawasahau.

 

Usiwahukumu watu bila ya kuwa na uhakika wa kile unachowahukumia. Mfano mdogo ni pale ombaomba amekuja kwenye ofisi yako wewe unamjibu kwa hasira “matapeli wamekuwa wengi sana siku hizi”. Kama huna cha kumsaidia mtu ni bora ukamwacha aende kwa Amani kuliko kumhukumu kwa kosa usilojua uhalisia wake.

 

Maumivu yeyote unayotengeneza ndani ya mioyo ya wengine ni miiba ambayo itakuja kukuchoma mbele ya safari yako.

Kila siku ifanye kuwa nafasi yako ya kupanda mbegu njema kwenye mioyo ya wengine.

Kila siku iwe ni nafasi ya kugusa maisha ya wengi kwa kupitia lile ambalo Mungu amekubariki nalo.

Kwa vyovyote vile kila tendo unalotenda kila siku linaweza kuja kuwa faida kubwa sana kwenye maisha yako baadae au hasara kubwa sana.

Kila unachosema kwa watu ni mbegu unapanda ndani ya mioyo yao kuwa makini na maneno yako. Maneno yako ndio yanakutafsiri ulivyo wewe. Maneno yako ndio yanasema wewe una tabia gani.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading