HATUA YA 273: Ipo Sababu

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Kila linalotokea kwenye maisha yako linatokea kwasababu usiwe mwepesi wa kulaumu au kulalamika wakati mwingine utajikuta unakosea. Kuna nyakati unaweza kuona umepatwa na mabaya Fulani kumbe sababu ya mabaya hayo ni kukuepusha na mabaya Zaidi.

Unaweza kuona mahusiano yako yanapitia changamoto na misukosuko hadi yakavunjika kumbe Mungu alikuwa anakuepusha na aibu ambayo ingekupata huko mbele. Usiogope wala kutikisika penda kujipa muda wa kutafakari kwanini yametokea.

Changamoto zozote unazopitia kwenye maisha usizione kama ni vikwazo wakati mwingine pia unakuwa unazuiwa kupita njia zako mwenyewe na Mungu anakuwa anataka akuonyeshe njia zake. Ukiona unafanya jambo linakwama kila wakati, umejaribu njia mbalimbali unakwama muulize Mungu.

Inawezekana umefeli shule, umekosa ada, umezaliwa kwenye familia maskini usiwe mnyonge, usijilaumu. Mungu anayosababu ya kukupitisha wewe huko. Kufeli kwako shule inawezekana ni hadithi Fulani Mungu anataka uwe nayo sasa wewe unataka kuindoa mipango ya Mungu juu yako.

Kukosa kwako ada na kushindwa kuendelea na masomo kunaweza kuwa ni sababu ya Mungu anataka kujiinua kwako sasa wewe unakuwa unamlaumu Mungu. Badala ya kulia na kulaumu mwambie kwamba unajua yeye anaweza. Mwambie mapenzi yake yatimie kwenye maisha yako.

Chochote kinachoendelea maishani mwako kina sababu, kuna mengi sana yanaendelea katika ulimwengu wa roho ambayo wewe hujajui lakini yeye anaona. Unapoona jambo limetokea usikazane kukimbilia kuwaza vibaya ona kwamba kuna jambo lipo nyuma ya pazia Mungu analitengeneza kwa ajili yako.

Hujaweza kwenda chuo kusoma mwambie Mungu akuonyeshe yeye anataka ufanye nini. Akikuonyesha kile anachotaka ukakifanya utafikia mafanikio makubwa na ipo siku utasimama utaeleza hukufika chuo lakini una mafanikio.

Badala ya kukata tamaa na kujiona huwezi mwambie Mungu akuonyeshe kile ambacho ameweka ndani yako. Kama wewe umeshindwa yeye hawezi kushindwa. Usimuachie yeye ukakaa unasubiri bali mwambie akuelekeze cha kufanya.

Kuna jambo unaweza kuliona ni bora sana machoni pako lakini yeye akaliondoa kwako ili upate bora Zaidi. Kuna mambo unaweza kuwa nayo yakawa ni sababu ya kuzuia Baraka zako kubwa Zaidi hivyo chochote kinachoondoka kwenye maisha yako hata kiwe kizuri kiasi gani jaribu kujua kusudi la kitu hicho kuondoka. Mwisho wa siku unakuja kugundua kwamba kumbe Mungu alikuwa amekuandalia kitu bora Zaidi. Wewe kuendelea kubaki na kile unachodhani ni kizuri kunakufanya ukose kile bora cha Mungu.

Siku zote Kuwa Karibu na Mungu mpe Maisha yako Ayaongoze.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading