HATUA YA 274: Unaufahamu Udhaifu Wako?

Kila binadamu kuna sehemu ambayo inakuwa ni rahisi sana kwake kufanya makosa hasa inapotokea ameingia katika mtego. Haiwezekani hata siku moja ukafikia ukuu kwenye kile unachokifanya kama huujui udhaifu wako.

Hakuna binadamu ambaye hajawahi kufanya makosa yaani nikiwa na maana kwenye kile unachokifanya kuna kitu ambacho kinakuwa sababu ya wewe kushindwa mara kwa mara. Ukiona wewe hauujui udhaifu wako basi ujue kuna siku utakuja kukuangusha ukiwa umeshafika mbali sana.

Kuufahamu udhaifu wako mapema ni nafasi kwako kufika mbali kimafanikio.

Kuufahamu udhaifu wako hakutakiwi kuwe sababu ya wewe kukata tamaa bali kusonga mbele Zaidi.

Ukifahamu kwamba wewe ukikaa karibu na vitu Fulani ni rahisi kushawishika Zaidi basi unakuwa kwenye nafasi salama Zaidi kwasababu una uwezo wa kuamua kutokuwepo karibu na vitu hivyo.

Udhaifu wako ni fursa kwako wewe kufanikiwa kama utaweza kuutumia vizuri.

Udhaifu wako ni anguko lako kama utashindwa kuutumia vyema katika namna chanya.

Watu wengi wabaya duniani wametokana na kutumia vibaya udhaifu walionao. Badala ya kutumia kama namna ya wao kuweza kutimiza kile kilicho ndani yao wamegeuka na kuwa watu wabaya Zaidi.

Soma: Ipo Sababu

Udhaifu wako ni nini?

Kile kitu ambacho kinakuangusha kirahisi kwenye makosa (dhambi). Embu tafakari ni jambo gani hasa huwa unalikosea sana? Ni kwanini unakosea? Hicho kinachokufanya wewe ukosee ndio udhaifu wako.

Ukiweza kugundua unakuwa umepata ushindi mkubwa sana. Ukiweza kutambua ni wapi huwa unaanguka kirahisi unaweza kutengeneza njia za kuepuka kuanguka hapo tena.

Ukishatambua ni wapi hasa panakufanya unakuwa chini hutaweza kujiruhusu kuwepo hilo eneo mara kwa mara.

Kama ni mawazo Fulani mabaya utakuwa unajizuia kufikiria au kuwepo kwenye sehemu itakayokufanya ufikirie hayo mawazo.

Usipoutambua udhaifu wako ni rahisi sana kutumbukia katika uharibifu.

Hakikisha unaufahamu udhaifu wako ili uweze kufika kule unakotaka kwenda.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

jacobmushi
Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.