Pamoja na mambo magumu unayopitia kwenye maisha yako kukataliwa, kuachwa, kusemwa vibaya tambua kwamba bado lipo Tumaini. Unapoona giza limeongezeka ujue kunakaribia kuwa asubuhi.

Kuna hadithi yako inatengenezwa kwa hayo unayopitia. Ipo siku utasimama na kutoa ushuhuda wa maisha uliyopitia. Ona magumu yako kama shule ya kukufikisha sehemu kuu Zaidi.

Hakuna mtu mkuu ambaye hajapitia kwenye njia ngumu. Hakuna kitu ambacho ni imara kimepatikana kirahisi.

Endelea kutazama kule unakotaka kufika, endelea kuona kuwezekana japo upo kwenye wakati mgumu.

Katika safari ya mafanikio kila mmoja atajaribiwa ili kujua kama ni kweli alidhamiria kuyafuata mafanikio au alikuwa na msisimko tu. Ni wachache wanaweza kuvumilia kupimwa huko na hatimaye wanaweza kufika kule walipokuwa wanapatamani sana.

Wengi huishia katikati na kurudi nyuma kule walipokuwa mwanzo. Hakuna namna nyingine ya kuweza kufikia kile unachokitaka kama hutoweza kuzivumilia na kuzishinda changamoto.

Hakuna njia rahisi ya kufika kwenye mafanikio na kama ingekuwepo basi watu wote wenye akili nyingi Zaidi yako wangeshaipitia hiyo. Lazima ukubali kwamba ugumu upo lakini Tumaini lipo.

Kama kuna wengi wameweza basi Tumaini la kufika kule unapotaka kwenda lipo. Hivyo usikubali kurudi nyuma. Hapo ulipo ni pagumu na patazidi kuwa pagumu kadiri muda unavyozidi kwenda.

Soma:  Unaufahamu Udhaifu Wako?

Haijalishi umefika wapi umri umekwenda kama tu bado upo hai hilo ni Tumaini kwamba una nafasi ya kufika kule unakotaka.

Jifunze kutumia muda wako vizuri. Kuna nyakati unaweza kufanya mambo makubwa ukiweza kuutumia muda huo vizuri utafika mbali mapema Zaidi ya wale ambao watafanya unachokifanya katika muda ambao ni mgumu.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading