Umejitoa kwenye nini?

Vitu gani unafanya kila siku na unatarajia kufikia makubwa miaka michache ijayo?

Malengo yako yanahusu nini Zaidi?

Vipaumbele vyako vimegusa kwa vile vitu ulivyochagua kuwa navyo au unavyotaka vitokee kwenye maisha yako?

Kama mpaka sasa hakuna jambo ambalo umejitoa kwa ajili ya hilo basi unapoteza muda na maisha yako.

Huwezi kusema maisha yako yana muelekeo kama hakuna jambo ambalo umeamua kulipa nguvu zako, muda wako, ujuzi wako, na maarifa hadi lilete matokeo makubwa maishani mwako.

Watu wengi wanaanza vitu na kuacha nusu au njiani kwasababu hawakujitoa kwenye vitu hivyo.

Unajua kama umeamua kusafiri huwezi kufika njiani ukasema unarudi kwasababu tu umechoka au safari imekuwa ndefu sana.

Sasa watu wengi wanachukulia maisha kama bahati mbaya Fulani hivi lakini unapaswa kuwa na vitu kwenye maisha yako umejitoa kwavyo hadi vilete matokeo kwenye maisha yako.

Jitoe kwenye kukuza Kiroho Chako.

Jitoe kwenye mahusiano yako.

Jitoe kwenye Kujifunza (Maarifa)

Jitoe kwenye Afya Yako.

Jitoe kwenye Kile unachopenda Kufanya.

Jitoe kwenye kuutafuta uhuru wa kifedha.

Jitoe kuyafanya maisha yako yawe bora.

 

Soma: Swali La Kujiuliza Unapojua Unachokitaka.

 

Utashindwa kwenda popote kama huna sehemu ambayo umejitoa hii ni kwasababu kila siku kuna vitu vingi vinatuvuta. Kuna fursa nyingi zinatuvutia. Kuna Imani nyingi zinatamani tuziamini.

Kuna wengi wanatamani uwe nao kwenye mahusiano. Kuna habari nyingi zisizo na maana. Kuna magonjwa mengi yanaweza kudhuru afya yako. Huwezi kuishi kwa uhuru kama huna pesa ya kutosha.

Fanyia kazi mambo haya hadi uone umefikia sehemu kubwa.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading