Kuna nyakati ili upate matokeo Zaidi ya unayopata sasa hivi utapaswa kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya, utatakiwa kuongea na watu ambao hujawahi au hujazoea kuongea nao. Hapo unakuwa umesogea mbele Zaidi ya uzio ambao ulikuwa umejiwekea.

Lazima utaanza kuona matokeo ya tofauti na uzoefu wa tofauti pia. Kuna hali zipo kwenye biashara zetu, mahusiano na kazi zetu kwa ujumla kwasababu tu hatujajaribu kwenda mbali Zaidi ya tulivyozoea.

Kama ulikuwa unazungumza na watu kumi kila siku kuhusu biashara yak oleo jiongoze ongeza namba ya watu ambao utatakiwa kuongea nao kwa siku. Kama kwenye mahusiano yako kuna vitu ulikuwa hujawahi kujaribu kumfanyia yule umpenda jaribu kufanya leo vitu ambavyo hujawahi kufanya na wala yeye hajawahi kutarajia umfanyie.

Unapoanza kufanya vitu ambavyo hujawahi kufanya utaona ugumu sana kwasababu sio vitu ulivyovizoea pia ni sawa na kujiumiza kwasababu unatumia nguvu Zaidi, muda Zaidi na akili Zaidi. Lakini baada ya muda utazoea na kuona inawezekana.

Ukishapata matokeo ndipo utagundua kumbe nilikuwa naweza kufanya hivi.

Vipo vitu vingi sana tunaweza kufanya kutokana na akili ambayo tumepewa na Mungu. Uwezo tulionao ni mkubwa sana endapo tutaweza kujilazimisha kujaribu kufanya Zaidi ya tulivyozoea kufanya.

Ukiweza kupiga hatua moja Zaidi usikwame tena hapo ukishazoea hiyo hatua jiongeze tena kusogea mbele Zaidi.

Soma: Mambo 5 yatakayokufanya Uendelee Kubakia Hapo Ulipo.

Usikubali kubakia wa kawaida, usikubali kuendelea kufanya vitu vilevile kila wakati. Jaribu vitu vipya, nenda sehemu ambazo hujawahi kufika, ongea na watu ambao hujazoea kuongea nao, na utaanza kuona tofauti kubwa kwenye kile unachokifanya. Utajifunza vitu vingi sana kwenye kusogea mbele Zaidi ya ulivyozoea.

Endelea mbele usikwame sehemu moja. Jaribu vitu mbalimbali lakini usitoke nje ya kusudi lako. Usitoke nje ya malengo ambayo umeweka.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading