Inawezekana umefika sehemu unaona kwamba haiwezekani kabisa. Umeanza kuona hali uliyonayo ndio ulitakiwa hivyo. Wakati mwingine umeshaanza na kusema kwamba wewe ulizaliwa uwe maskini.

Jambo moja unapaswa kujiuliza ni kwamba kama kungekuwa hakuna kushindwa, hakuna changamoto, hakuna ugumu wowote ni jambo lipi hilo ungechagua kulifanya hadi ufikie mafanikio makubwa.

Ni kitu gani ungependa dunia ikutambue nacho?

Ni kipaji gani ungependa kukitimiza?

Ukipata majibu unapaswa kutambua kwamba inawezekana. Haijalishi changamoto zipo za kiasi gani lakini bado inawezekana.

Ukiweza kupata jibu anza kuchukua hatua za kila siku kufanyia kazi ndoto yako na jibu lako hadi ndoto yako iwe kweli.

Jitoe kikamilifu kwa hiyo ndoto yako hadi uone mafanikio. Kuwa bora, weka juhudi za kutosha.

Inawezekana kabisa ndoto yako ikatimia hata kama hali unaona ni ngumu sana.

Usikubali vikwazo vikurudishe nyuma, vipo ili kukufanya imara.

Usikubali watu wawe sababu ya wewe kukata tamaa usiwasikilize maneno yao

Inawezekana kile ambacho Mungu ameweka ndani yako kikatimia na kwenda kugusa maisha ya wengi.

Soma: Umejitoa Kwenye Nini?

Imewachukua watu miaka mingi sana kuweza kufika sehemu ya juu ambapo watu wengi wanawatazama. Hivyo na wewe usikubali kabisa kukata tamaa kwenye kile ulichoamua kufanya.

Endelea mbele, jitie nguvu ipo siku yako na wewe utatoa shuhuda. Ipo siku na wewe wengi watajifunza kupitia safari yako. Haijalishi unapitia nini kwa wakati huu kinachoangaliwa ni uwezo wako wa kuvumilia hadi uifikie ndoto yako.

Watu wakuu wameweza kuzishinda changamoto kubwa ndio maana wanaweza kuendelea kusimama kule walipofika.

 

Jifunze na Ufanikiwe kwenye Ujasiriamali, na Biashara.

Tambua Kusudi la wewe kuwa Hai Ufanikiwe.

Mbinu na Kanuni za Utajiri na Mafanikio.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

2 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading