HATUA YA 279: Ni Ushindi Mdogo, Mdogo.

Kwa kawaida hakuna kitu kimoja unachoweza kufanya kikakufikisha kule unakotaka moja kwa moja. Hapa nikiwa na maana ya kwamba ukitaka kuvuna mahindi gunia mia unatakiwa upande mashimo mengi sana ya mahindi kwenye mashamba. Huwezi kutegemea shimo moja likuletee hayo mahindi hata kama utaweka mbolea ya kutosha, ukahakikisha hayaguswi na wadudu, bado shimo moja halitoshi kuleta gunia mia.

Unapaswa kujua ni vitu gani unatakiwa kufanya ili yakuletee yale matokeo unayotaka. Lazima uweke juhudi na kila mchango mdogo unaopata ndio mkusanyiko wa ushindi wako mkubwa.

Watu wengi tunatamani kufika mbali lakini wanataka kufika kimiujiza. Wengine ni pasipo kujua wanabaki wanasubiri jambo Fulani litokee kwenye maisha yao. Kwa bahati mbaya sana unakuta jambo hilo wanalosubiri sio wao wanalisababisha litokee hivyo wanaendelea kusubiri na kusubiri.

Ukiweza kutambua kwamba nini unataka na ukaanza kufanya jambo moja moja hata kama ni dogo sana lakini likawa linahesabu na kukusogeza karibu na ushindi wako.

Jiwe kubwa halipasuliwi kwa kupiga nyundo mara moja. Linapasuka kwa kurudia rudia kupiga jiwe kwa ufundi wa kila aina hadi lenyewe linapasuka. Ukisema umepiga nyundo moja ukasubiri lipasuke hakuna kitakachotokea.

Jua unachokitaka na hakikisha kuna kitu unakifanya ambacho kinakupa matokeo hata kama ni kidogo kiasi gani lakini yanakupeleka kule kwenye ushindi mkubwa.

Soma: ZIFAHAMU TABIA 4 ZINAZOWAZUIA WAJASIRIAMALI VIJANA KUFANIKIWA.

Jiulize unataka nini?

Unakataka kuwa nani?

Je unachokifanya sasa hivi kitakupelekea kupata yale matokeo unayotaka?

Kinakupeleka kule kwenye ndoto yako kubwa?

Unataka kuwa na ndoa nzuri maisha unayoishi sasa hivi yanasemaje?

Unataka kuwa na uhuru wa kifedha je tabia zako za sasa hivi za fedha zikoje?

Kama utaweza kujibu maswali hayo unaweza kujua unapokwenda ni wapi kulingana na uanchokitaka. Hakikisha matendo yako ya sasa hivi yaelezee kwako mwenyewe kule unapokwenda. Hata kama watu wa nje wasipokuelewa lakini wewe uwe unaelewa uendako.

Jifunze na Ufanikiwe kwenye Ujasiriamali, na Biashara.

Tambua Kusudi la wewe kuwa Hai Ufanikiwe.

Mbinu na Kanuni za Utajiri na Mafanikio.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue Reading