HATUA YA 280: Watu Wengi Wamekosa Kitu Hiki ndio Maana Hawafiki Popote.

Kuna msemo mmoja wa wahenga unasema “mazoea hujenga tabia” ni kweli lile jambo ambalo umezoea kulifanya mara kwa mara linakuwa tabia yako. Lakini kitu cha kushangaza sana ni kwamba wengi wanafanya mambo ambayo hawayataki kwenye maisha yao.

Watu wengi wanafanya mara kwa mara yale mambo yanayoleta umaskini na wakati mwingine hata maradhi. Mambo mazuri yamekuwa ni magumu sana kufanya kwa watu kuliko hata mabaya.

Mfano ni rahisi sana mtu kuzoea kuchelewa kuamka kuliko kuamka mapema.

Ni rahisi sana mtu kujenga tabia ya kuahirisha kuliko tabia ya kufanya jambo kwa wakati.

Ni rahisi sana mtu kutumia pesa yote anayopata kuliko kuweka akiba.

Wengi watakwambia kuweka akiba ni ngumu sana, hii biashara nitaanza siku nyingine. Hili jambo nitalifanya siku nikiwa na muda. Nitaweka akiba nikipata pesa nyingi.

Mwisho wa siku unakuta tabia ambazo umezibeba ni zile mbovu kuliko tabia ambazo zingeleta mafanikio kwako.

Soma: Unataka Kwenda Hatua Nyingine?

Yote Haya Yanasababishwa na Ukosefu wa Nidhamu.

Ukikikosa nidhamu maisha yako yanakuwa ni ya hovyo sana. Huwezi kufanya jambo likafikia mwisho kama huna nidhamu. Huwezi kufikia ndoto zako kubwa kama huna nidhamu.

Umesema utafanya jambo Fulani kama kweli una nidhamu huwezi kukubali sababu nyingine zikuzuie. Kama kweli una nidhamu huwezi kuacha kufanya kile ulichosema unafanya kwasababu ratiba zimekuwa ngumu.

Maisha bila ya nidhamu ni ngumu kufikia mafanikio.

Ndugu yangu ukitaka mabadiliko jenga nidhamu.

Ukitaka mafanikio jenga nidhamu.

Acha kujidanganya mwenyewe, kama huna nidhamu utapotea.

Fanya kile ulichosema utafanya hata kama kumetokea hali ya aina gani.

Umaskini unaletwa na uksoefu wa nidhamu,

Jijengee nidhamu kwenye kile ulichoamua kukifanya.

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading