HATUA YA 281: Kuna Mtu Anakuamini?

jacobmushi
3 Min Read

Kama utaishi hapa duniani halafu ukakosa watu ambao watakuamini utaishi Maisha magumu sana. Hii ni kwasababu kuna baadhi ya mambo unapoyafanya lazima uwe una watu wanaokuamini. Wanaojua sifa zako za ufanyaji kazi.

Unaweza kuwa unalalamika huna mtaji wa kuanza biashara lakini mtaji ungeupata kama ungekuwa na watu watano tu wanaokuamini. Unaweza kulalamika Maisha magumu hakuna fursa lakini fursa ungeziona na ungepata mpenyo tu kwa kuwa na watu ambao wanakuamini.

Kuna hatua huwezi kuzivuka kama huaminiki. Kuna mahali huwezi kupata nafasi ya kuonyesha kile ulichonacho kwasababu huaminiki.

Kitu cha kuanza kujenga sasa kwenye Maisha yako ni kujenga watu ambao wanakuamini. Na watakuamini kwasababu wewe ni mtu ambaye unaishi maneno yako. Ukisema unafanya jambo Fulani unafanya.

Soma: Watu Wengi Wamekosa Kitu Hiki ndio Maana Hawafiki Popote.

Wengi tunashindwa kuaminika kwasababu tuna maneno mengi na vitendo vichache. Unaongea sana kuliko unavyotenda. Watu wanashindwa kuamini tena maneno yako.

Hata ukiwa na shida wanaona huu utakuwa usanii tu huu. Kwasababu ya mambo unayosemaga utafanya lakini hufanyi.

Ili uweze kujenga uaminifu lazima uwe na tabia hizi:

  • Tekeleza unachokiahidi kwa watu.
  • Ishi maneno yako.
  • Wafanye watu wakutegemee kwa kile unachokifanya.
  • Fanya vitu bora kila wakati.
  • Usiwaangushe watu.
  • Kuwa mtu wa hapana ni hapana na ndio ni ndio. Unajikuta kwenye kuingia makubaliano Fulani ukatakiwa kusema hapana basi iwe hapana kweli, na pale unaposema ndio iwe ndio kweli. Kuna tabia unaweza kuwa nayo watu wakashindwa kukuamini. Unasema hapana halafu baadae unakuja kusema ndio. Unasema ndio halafu baadae unakuja kusema hapa.
  • Kuwa mwaminifu kwa vitu vidogo.

Vitu vidogo vidogo ambavyo unasema hawatajua ndivyo vinakuangusha kwasababu kuna watu wanavitazama na kuvithamini vile ambavyo wewe unaona ni vidogo.

  • Kuwa mnyenyekevu.

Usiwe mnyenyekevu tu kwasababu una uhitaji Fulani huo utakuwa ni unafiki. Unyenyekevu uwe tabia yako wakati ukiwa nacho na hata wakati ukiwa huna chochote.

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
1 Comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading