Kama kuna jambo umekuwa unaliogopa sana kulifanya katika Nyanja ya mafanikio hiyo ni ishara ya kwanza kabisa kuonyesha kwamba jambo hilo litaleta matokeo makubwa kwenye Maisha yako.

Woga unakuja kwasababu kuna kitu cha tofauti utakwenda kufanya. Kwasababu ya akili yako kutokuzoea jambo hilo la tofauti itakuaje zinakuwa nyingi na kukufanya wewe ushindwe kufanya maamuzi.

Unachukua hatua na kuanza unajikuta umetoka katika ile hali ambayo umekuwa unaizoea na kwenda hatua ya ziada mbele. Baada ya kuchukua hatua utaanza kuona kuna ujasiri Fulani umeongezeka.

Jambo unalogopa kufanya ndio limebeba muujiza wako. Kuna kitu cha tofauti utakipata utakapoanza kuchukua hatua.

Hata kama itatokea ukashidnwa basi ujue utakuwa umeongezeka uzoefu kwenye Maisha yako.

Siri iliyojificha kwenye mambo unayoogopa kufanya ni kwamba ndio yamebeba milango yako ya mafanikio. Ufunguo unao wewe wa kuchukua hatua usipochukua hatua kamwe huwezi kutoka hapo ulipo sasa hivi.

Soma:  Kuna Mtu Anakuamini?

Kama kinachokupa woga hakiwezi kuondoa uhai wako basi unatakiwa ukifanye bila ya kuangalia nani atasema nini, au watu watakuonaje au kushindwa.

Ushindi wako umefungwa kwenye woga wako. Achana na woga anza kufanya.

Wale unaowaogopa hakuna wanakuongezea kwenye Maisha yako.

Vile unavyozani labda watu wanafikiri kuhusu wewe wala hawana muda huo  ni mawazo tu uliyojijengea kwenye akili yako.

Ni wakati wako sasa kuondokana na woga, ulikuja duniani mwenyewe na utaondoka mwenyewe.

Uliwakuta watu hapa duniani na wengine huenda ukawaacha pia hivyo hakuna haja ya kuogopa na kupoteza nafasi yako ya kuishi ukifanya mambo ambayo ulipaswa kufanya.

Hofu ya kushindwa isikuzuie kwasababu hakuna alieshinda bila ya kuumia mahali. Hakuna aliefikia ushindi mkubwa bila ya kupitia sehemu yenye miiba.

Mtu yeyeote au kitu chochote kisiwe sababu ya wewe kuacha kufanya kile ambacho moyo wako unafurahia.

 

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading