Mtazamo wako ndio unaamua ukubwa au udogo wa matatizo yako.
Mtazamo wako ndio unaamua wewe ushinde au ushindwe kwenye changamoto unazopitia.
Mtazamo wako ndio unakufanya wakati mwingine ukosane na watu kutonakana na namna unavyowatafsiri.
Ukiweza kubadili mtazamo wako juu ya mambo unayoyapitia unaweza kupiga hatua kubwa sana.
Kama kiongozi unaweza kuwaharibu kabisa wale unawaongoza kutokana na mtazamo wako ulivyo.
Tukitazama katika Biblia wana wa Israel walipotaka kwenda Yeriko walituma wapelelezi wakaipeleleze nchi. Kati ya wale wapelelezi kulikua na wenye mitazamo ya tofauti kwa jinsi walivyoiona nchi. Kuna walioona kwamba nchi ni ya kwao yaani watakwenda kuimiliki. Na kuna walioona wanakwenda kushindwa. Walipowatazama wale watu ndani ya Yericko wakajiona wao wamekua kama mapanzi tu. Lakini wengine waliona kushinda.
Ukiwa na watu wenye mitazamo ya kushindwa katika maisha yako watakuharibu na watafanya ufanane nao. Haijalishi ukubwa wa tatizo kikubwa ni jinsi wewe unavyolitazama tatizo. Kuna wakati unaweza kupita kwenye changamoto ukaona kama ndio umefika mwisho, halafu unaenda kumweleza mtu anakushangaa. Anakwambia si ungefanya hivi na hivi, ukiangalia anachokuambia ni kweli ukifanya kingeleta mabadiliko. Kilichokua kinakufanya ushindwe ni mtazamo wako tu.
Daudi hakumshinda Goliathi kwasababu ya uzoefu wa kivita kwani hakuwahi kupigana vitani. Mtazamo wake juu ya Goliati ndio ulimwezesha ampige. Hata wewe haijalishi upo kwenye mambo makubwa na magumu kiasi gani hebu jaribu kufikiri tofauti leo uone ni jinsi gani utakavyobadilisha.
Badilisha mtazamo wako, anza kuona ushindi hata wakati unapitia kwenye magumu. Kiri ushindi hata pale unapoona unakwenda kuanguka. Hakikisha unazungumza kile unachotaka kuona kinatokea kwenye maisha yako.
”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com