Pamoja na kwamba tunapambana kila siku ili kuweza kuyafanya Maisha yetu yawe bora vipo vitu vya muhimu sana tunapaswa kuvitazama Zaidi.

Unaweza kumiliki utajiri wa kila mali inayoonekana kwa macho lakini kama humiliki akili wewe ni maskini kama maskini wengine.

Akili peke yake ndio mali ambayo unaimiliki na hakuna binadamu ambaye anaweza kukuibia.

Watu wengi tunatumia muda mwingi kufikiria Zaidi kuhusu mali zetu za nje na kusahau kabisa juu ya akili zetu.

Hivi unajua bila ya akili wewe usingekuwa na chochote. Bila ya akili usingeweza kutunza chochote ulichonacho sasa hivi.

Bila ya akili wewe tungekuita masikini au kichaa.

Ni mara ngapi unapata muda wa kuiboresha akili yako?

Ni mara ngapi unapata muda wa kuilisha akili yako?

Ni mara ngapi unainunulia vitu bora akili yako?

Ukishindwa kujua umuhimu wa akili yako huwezi kutambiua ni vitu gani vinapaswa kuwekwaa ili kuitunza. Wengi wetu akili zimekuwa kama jalala maana kila uchafu unawekwa. Kila kilicho kichafu kinawekwa bila kujali kinakwenda kuharibu kwa kiasi gani.

Akili yako ndio yenye uwezo wa kukurudishia pale ulipokuwa mwanzo endapo utapoteza kila kitu ulichonacho sasa hivi. Mungu alipokuumba alikukamilisha ameweka kila kitu ndani yako. Unachopaswa ni kumuomba wakati mambo yanapokuwa magumu.

Usizitegemee akili zako mwenyewe ukamsahau aliezikupa. Siku zote mwombe pale unapoona umeshindwa. Siku zote kuwa karibu nae atakusaidia.

 

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

One Response

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading