Siku zote ili upate kile unachokitaka inatakiwa unachokisema kiendane na unachokifanya. Na kama ukiona maneno yako ni tofauti na unayoyafanya kila siku ujue umeshapotea.

Kama unapenda mafnikio anza kufanya vitu vitakavyokupeleka kwenye mafanikio. Kama unataka pesa acha kufanya starehe achana na msemo usemao tumia pesa upate pesa badala yake anza kutumia pesa kwenye vitu vitakavyokuletea pesa Zaidi.

 

Vijana wengi siku hizi kitu kikubwa kinachotkwamisha ni starehe. Wengi wanaita kula ujana. Tunasahau pia kila jambo linahitaji kiasi hata kama ni wakati wake. Chochote ukizidisha kinaleta madhara hata pesa ukiwa nazo kuliko uwezo wako zinaleta uharibifu. Angalia kile unachokifanya unakifanyaje kwa kiasi na kutumia maarifa.

Badilisha sasa matendo yako yaelekee kwenye kile unachokihubiri utaanza kuona matokeo. Badilisha vile vitu visivyo na matokeo ya baadae. Vitu vinavyokupa raha hapo hapo habari imekwisha. Vitu hivi pia vinaongoza katika kukurudisha nyuma. Vitu vinavyokupa raha ya muda mfupi vitakuletea matokeo mabaya ya muda mrefu jaribu kupunguza vitu vya namna hii.

Soma:Mambo 5 yatakayokufanya Uendelee Kubakia Hapo Ulipo.

Muda wako mwingi tumia kujiendeleza kama unahisi huna cha kufanya. Tafuta kitabu soma hata kama hauko kwenye mudi (haujisikii). Sikiliza na angalia  vitu vinavyojenga ufahamu wako. Punguza au achana na kampani zisizo na matendo ya mafanikio. Ukikaa na rafiki mlevi atakufundisha ulevi. Ukikaa na mzinzi atakufundisha uzinzi. Ukikaa na anaejifunza atakufundisha kujifunza lakini ukimletea tabia zako mbovu atakukimbia.

Ukiona upo na watu wasio tambua thamani ya muda watu hao ni wa kukimbia kabisa maana watakuletea hasara kwenye maisha yako. Muda ndio kila kitu kwenye kile unachokifanya ukishindwa kupangilia muda wako utapotea. Wewe kila anaekuja akakuletea ratiba zake wewe unaingia kwenye ratiba za wengine. Jiulize ni wangapi wanaingia kwenye ratiba zako wewe. Wakati unasoma vitabu wakati unataka kufanya mambo yako ni wangapi wanaingia kwenye ratiba zako.

Kua mtu wa mipango na vitu vyovyote visvyokuletea matokeo bora kwenye malengo na ndoto zako achana navyo. Pangilia siku, week, mwezi na hata mwaka Mungu akiona una mipango mema hawezi ruhusu adui akuguse hawezi ruhusu mabaya yakukute atakulinda.

 

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading