Unachokifanya sasa hivi kama kinatoka ndani ya moyo wako upo tayari kukifanya hadi unakufa hata kama hutapata chochote? Hili limekuwa ni swali moja gumu sana kujua kama watu wanaosema wanapenda wanachokifanya wanapenda kweli au ni maneno.

Kama utakosa chochote kusifiwa, kulipwa, kupongezwa na bado ukaendelea kufanya inaonyesha kweli umejitoa kufanya kile unachokifanya.

Je upo tayari kukataliwa?

Kuna nyakati utafanya jambo na watu ambao ulitarajia wakupongeze ndio wakawa wa kwanza kukusema vibaya. Je upo tayari kukubaliana na kukataliwa na bado ukasonga mbele?

Je upo Tayari Kuumizwa?

Kuna watu wengi wanatuzunguka tunawaamini na kuwapa sehemu za muhimu kwenye Maisha yetu na baadae wanaondoka na kutuacha tukiwa hatujui tena cha kufanya. Umemkaribisha mtu kwenye Maisha yako ukijua mtaenda nae hadi mwisho ukaufunua moyo wako akayajua yote yaliyopo ndani yako kisha akakukimbia na kukuacha. Upo Tayari?

Upo Tayari Kuonekana Unaringa?

Kuna nyakati unaweza kusema hapana kwenye mambo ambayo hayana faida yeyote kwenye safari yako ya Maisha na bado watu wakaona wewe unajiona umeshafanikiwa unawadharau. Je upo tayari kupitia hayo na ukasonga mbele?

Kama upo tayari kupitia hayo yote na mengine mengi utakayokutana nayo njiani basi twende mwaka 2018 kwa nguvu Zaidi ili tuweze kupiga hatua kubwa Zaidi.

Soma: Unachokisema na Unachokifanya

Ni wachache sana wanaweza kutekeleza vile vitu wanavyosema na mimi natamani sana wewe Rafiki yangu uwe mmoja wa hao watu. Wengi wanaishia kusema lakini wachache sana wanamaanisha wanachokisema na kwenda kukifanyia kazi.

Twende 2018.

” Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading