Kuna baadhi ya watu huwa unawakuta kwenye kila kitu. Kila kinachokuja kipya anakuwepo ndani yake.

Kila fursa mpya unayotokea unataka ufanye. Mafanikio hayatakuja kwa kufanya vitu vingi bali kwa kufanya mambo machache hadi yakakuletea matokeo.

Jifunze kufanya jambo moja hadi lilete matokeo. Nikwambie ukweli kama unachokifanya sasa kuna watu wanaendelea kukifanya na wana mafanikio makubwa basi jifunze kujipa subira.
Waulize wamechukua muda gani hadi kufika pale walipofika ndipo uchukue maamuzi ya kuacha.

Usikubali kufanya maamuzi kwa kutumia hisia tumia akili. Mara nyingi mtu anapokujia na hadithi nzuri za watu waliofanikiwa kwenye biashara ili kukuvutia wewe uingie kuwa makini sana usije kufanya maamuzi kwa makosa. Kama mtu amefanikiwa mwambie akuonyeshe njia aliyopitia gharama alizolipa hadi kupata alichokipata.

Mafanikio yeyote ambayo hayana gharama unayolipa usikimbilie. Kubali kuwa na subira kwenye kile uanchokifanya. Kama hakuna mafanikio hakikisha unajua unapokosea. Kama kuna wengine wanafanya vizuri basi wewe kuna mahali unakosea.

Ukishindwa kufuata kanuni ambazo zipo tangu kuumbwa kwa ulimwengu utajikuta umefanya mambo mia moja lakini hakuna kilichobadilika kwenye Maisha yako. Huwezi kupanda mbegu moja ya maharage halafu utarajie kuvuna gunia.


Sio kila Vita unatakiwa Upigane, Sio Kila fursa inayokuja ni ya Kuchukua. Tumia akili usitumie hisia kufanya maamuzi.

USHAURI: Kama unajua kwanini upo hapa duniani (Kusudi). Na tayari Una maono ya kufika sehemu kutokana na kusudi lako. Chochote kinachokuja mbele yako cha kufanya hata kivutie kiasi gani inakua rahisi sana kufanya maamuzi sahihi. Utakachokiangalia wewe ni KUSUDI LAKO NA KULE UNAPOKWENDA (MAONO). Kama kilichokuja mbele yako hakiendani na hivyo vitu viwili na wala hakina matokeo bora yeyote kwenye maono yako utaacha. Ni muhimu sana ujue unapokwenda ili usichukuliwe na kila upepo.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading