HATUA YA 290: Heri Ya Mwaka Mpya

jacobmushi
2 Min Read

Habari Rafiki yangu mfuatiliaji wa Makala hizi za HATUA. Kila mmoja anayofuraha na jambo la kusema asante kwa Mungu alietupa uzima na tumeweza tena kuona mwaka huu 2018.

Pamoja na mengi sana ambayo ulipitia mwaka jana magumu kwa namna yeyote ile tafuta mema ambayo unaweza kusema ni shukrani kwa Mungu. Kwanza kuwepo hai pekee ni jambo kubwa sana la kushukuru kwa Mungu.

Mwaka 2018 umepanga kufanya vitu gani? Unataka kitokee nini kwenye Maisha yako?

Chochote unachotaka inawezekana kukipata kama tu utaamua kwenda tofauti na wengi wanavyofanya. Ukitaka kupotea ni uchague kufanya kama ambavyo kila mtu anafanya. Ukifanya kama kila mtu anavyofanya huwezi kupata matokeo tofauti ya wao.

Njia moja ambayo unaweza kuitumia kufanya vitu kwa tofauti na wengi ni kuchagua kufanya kwa ubora Zaidi yao. Chochote unachogusa na mikono yako hakikisha kinakuwa bora Zaidi kinyume nah apo huwezi kusema umefanya utofauti.

Tofautishwa na ubora kwenye mambo yako. Unaweza kufanya jambo zuri sana lakini ukishindwa kuwa bora mambo yanakuwa ya hovyo kama wengine.

Jambo la mwisho napenda kukwambia hujaja duniani kurudia mafanikio ya wengine. Mungu amekuleta uje ufanye mambo ya tofauti, utengeneze njia mpya na za tofauti na wengine. Usikubali kabisa kurudia kule walipopita wengine tengeneza historia yako.

Nikushukuru sana kwa kufuatilia Makala hizi kwa mwaka mzima 2017. Mwaka huu tutaanza na kitu kingine kipya kabisa ambacho tutajifunza pamoja kila siku.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading