HATUA YA 292: Ni Rahisi Sana Lakini…

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Ni rahisi sana kulalamika Maisha ni magumu,

Ni rahisi sana kutoa sababu nyingi zilizofanya ushindwe,

Ni rahisi sana kuendelea kuishi Maisha yale yale uliyoyazoea,

Ni rahisi sana kutumia muda wako kufanya mambo ambayo hayana mchango wowote kwenye Maisha yako.

Ni rahisi sana kutumia muda wako kufuatilia Maisha ya wengine na huku ukiwa umeyasahau ya kwako.

Ni rahisi sana kutafuta mtu wa kumbebesha matatizo yako kwamba ni yeye ameyasababisha.

Sasa kitu kikubwa hapo ni kwamba vitu vyote hivyo virahisi hakuna hata kimoja kinachoweza kukutatulia matatizo yako. Ukisema hali mbaya ya pesa uliyonayo imesababishwa na mtu Fulani, hakuna kinachobadilika. Unabaki pale pale ulipokuwa tangu mwanzo.

Kitu cha kushangaza sana ni kwamba bado watu wanachagua kufanya vitu ambavyo ni virahisi kwenye Maisha yao. Hakuna anaetaka kufanya mambo ya tofauti, hakuna anaetaka kuchukua hatua ili kubadili Maisha yake.

Ukweli ni ngumu sana kuishi Maisha ambayo hujayazoea. Kuacha kufuatilia Maisha ya watu wengine. Kuacha kulalamika, kutoa sababu. Sio rahisi kuanza kujitoa kusoma vitabu na kufanyia kazi yale ambayo unajifunza.

Ni ngumu sana kuwaondoa watu ambao siku zote wanalalamika Maisha ni magumu kwenye Maisha yako. Sio kitu kirahisi kuanzisha biashara kama mshahara wako hautoshi. Sio rahisi kukaa mbali na marafiki ambao mara nyingi mmekuwa mnakaa mnapiga hadithi vijiweni.

Lakini pamoja kwamba ni ngumu kuna matokeo makubwa kwneye Maisha yako. Hutabaki kama ulivyo kuwa mwanzo. Maisha yako yatapanda kwenda viwango vingine. Siku zote vitu ambavyo vinafanywa na wengi havina matokeo makubwa. Vile vigumu ni wachache ndio wamejitolea kufanya na ndio wenye mafanikio.

Ukiamua kubadilika INAWEZEKANA. Ukiamua kuanza Maisha mapya inawezekana, marafiki wasio kushauri na kukufanya usonge mbele hao hawafai. Watu wasio na mawazo makubwa juu ya Maisha yao sio wa kuendelea kukaa nao tena. Chukua hatua sasa anza kufanya vitu vya tofauti ili ubadili Maisha yako.

NDOTO YAKO INAWEZEKANA, AMKA SONGA MBELE.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668/0755192418,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading