Do not spoil what you have by desiring what you have not; remember that what you now have was once among the things you only hoped for. -Epicurus

Moja ya mambo ambayo yanawafanya watu washindwe kuishi Maisha ya furaha hapa duniani ni kutokujua ni vitu gani wanataka. Unaweza kukuta mtu anapata kila anachokitafuta lakini bado hawezi kupata muda wa kukaa chini na kufurahia kile anachokipata.

Lazima ujue kwamba kile kidogo unachofanikiwa kupata leo kilikuwa ni mojawapo ya vitu ulikuwa unatamani sana kuwa navyo. Utakuwa unapoteza maana ya kuvitafuta kama huna muda wa kuvitumia na kuvifurahia.

Haijalishi ni matokeo madogo kiasi gani umepata lazima ujue kwamba hayo pia ulishawahi kutumaini kuyapata.

Unaweza kujikuta umeishi Maisha yako yote ukitafuta tu na ukakosa muda kabisa wa kukaa na kuangalia kile ulichokuwa unakifanya.

Sababu kuu inayofanya wengi waishie kuwa watafutaji Maisha yao yote ni kuangalia Zaidi walichokikosa kuliko kile ambacho wameshapata. Ukitazama ambavyo huna utaviona vingi sana, ukitazama ambavyo umeshapata tayari vile vile utaviona vingi mno.

Hii haina maana kwamba uache kutafuta kabisa bali ni kukufanya wewe uweze kuona thamani ya vile ambavyo tayari umeshavipata. Ona Maisha yako bado ni bora kwa vile ambavyo tayari unavyo huku ukiendelea kutafuta.

Ukiweza kuwa na mtazamo huo huwezi kuwa mtu wa kulalamika na asiye na shukrani. Ukiweza kuona wingi wa vile ambavyo umeshavipata utaweza kuishi Maisha bora hapa duniani.

Nothing is enough for the man to whom enough is too little. – Epicurus

Nakutakia Mafanikio Mema.

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Life Coach,

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading