Sometimes by losing a battle you find a new way to win the war. Donald Trump.
Kwenye moja ya vitabu vya Rais wa Marekani Donald Trump amewahi kusema kuna nyakati tunaposhindwa ndipo tunapata njia za kushinda vita.
Wakati mwingine tunayachukua makossa yetu na kuyafanya kama alama mbaya juu yetu. Hii inatokana na namna ambavyo uliambiwa tangu ukiwa mdogo. Ulipokuwa unakosea ulionekana kama mjinga Fulani asiye na akili. Hivyo hata sasa unaona ukikosea basi na wewe utakuwa huna akili.
Ukweli ni kwamba wewe ambaye umethubutu kujaribu na ukakosea una uwezo mkubwa sana kuliko yule ambaye hajafanya chochote. Haijalishi umekosea mara ngapi kukosea kwako kumekufanya ugundue njia ambazo sio sahihi za kukufanya ufanikiwe.
Usikubali watu wakuone wewe hufai na huwezi kwasababu ya jambo uliloshindwa. Usikubali wewe mwenyewe kupokea hali hiyo ndani yako kwani inaweza kuwa sababu ya kukwamisha kufanya mengine.
Unaweza kukosa ujasiri wa kujaribu mengine kwasababu ya ufahamu huu kwamba wewe hufai tena kwasababu ulikosea kitu Fulani.
Kwenye safari ya mafanikio kuna wakati unapitia kushindwa kwa kila unalofanya lakini unapaswa kujitia nguvu kwamba kama umejaribu njia Fulani ukashindwa basi njia hiyo siyo sahihi unatafuta njia nyingine.
Unapofanya makosa ndipo unagundua namna ya kufanya kwa usahihi Zaidi. Kamwe usikubali kosa lako liwe sababu ya kukukandamiza chini Zaidi.
Unapokosea jambo inatakiwa iwe sababu ya wewe kujua njia nyingine bora Zaidi.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Author | Trainer | Entrepreneur
Simu: 0654 726 668 |0755192418,
Twitter: @jacobmushitz
Instagram: @jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com