HATUA YA 296: Vile Unavyofikiri Juu ya Vitu Ndio Inaamua Furaha au Huzuni.

jacobmushi
2 Min Read

Very little is needed to make a happy life; it is all within yourself, in your way of thinking. -Marcus Aurelius.

Mwanafalsafa huyu anatuambia ni vitu vidogo sana vinakukuhitaji ili uwe na furaha ya Maisha, na vitu hivyo vipo ndani yako katika namna unavyofikiri.

Furaha au huzuni hailetwi na matukio yanayotokea bali ni namna ambavyo tunaamua kufikiri juu yay ale matukio yenyewe. Linaweza kutokea tukio baya sana kwenye Maisha ya watu wawili mmoja akabaki ana hali yake ya kawaida na mwingine akachanganyikiwa kabisa. Yote hayo yanatokea kwa vile tunavyofikiri tu.

Unaamua mwenyewe kuwa na furaha, vilevile unaamua mwenyewe kuwa na huzuni. Matukio na vitu vya nje vinaweza kuwa vichocheo tu ya hali yako ya ndani.

Usikubali Maisha yako yakaendeshwa na matukio ya nje bali wewe mwenyewe unavyoamua yawe. Ukiyaruhusu matukio ndio yawe kiongozi wa namna unavyokwenda utakuwa mtu wa kuchanganyikiwa kila nyakati.

Haijalishi unapitia jambo gani kubwa kutokuwa na furaha hakubadilishi jambo lile. Umepata msiba mzito wa mtu wa karibu sana kwako kuwa na huzuni kubwa sana hadi ukashindwa kula au ukaugua kabisa hakubadilishi chochote kwenye tukio lile.

Unachopaswa kujua ni kwamba hupaswi kuumia au kushindwa kuishi vyema kwa matukio ambayo huwezi kuyadhibiti.

Fanya lile ambalo linakupasa mengine mwachie Mungu.

Jambo la mwisho penda kuwa mtu ambaye anatazama kwa upande chanya kwenye kila jambo ambalo linatokea utajikuta unaishi Maisha ya toauti sana na wengine.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading