“All you need in this life is ignorance and confidence; then success is sure.”
― Mark Twain

Samuel Langhorne Clemens ambaye anajulikana zaidi  kwa jina la Mark Twain aliwahi kusema; kitu ambacho unakihitaji kwenye Maisha yako ili ufanikiwe kwa hakika ni ujinga na ujasiri. Hii ina maana ya kwamba wewe ukubali kwamba hujui chochote halafu uwe na ujasiri wa kujifunza kwa kila mtu aliekutangulia na alieko nyuma yako.

Tatizo la watu wengi hawako tayari kuonekana kwamba hawajui, yaani hawako tayari kuonekana kwamba wao ni wajinga. Ukweli mjinga ni yule mtu ambaye hajui kitu. Mtu pekee mwenye nafasi ya kujua vitu vingi ni mjinga ambaye amejitambua kuwa yeye ni mjinga na akawa tayari kujifunza.

Kama tutaweza kukubali kuwa tu wajinga kwenye mambo mengi na tukawa tayari kujifunza kwa wengine ambao wameshafanya Zaidi yetu tutafanikiwa. Ujinga ni kitu kibaya pale ambapo mjinga anakuwa hajitambui kabisa kwamba yeye ni mjinga ambapo hapo sasa anakuwa mpumbavu.

Mjinga ambaye ni mjasiri anaweza kufanya mambo makubwa kwasababu anatamani atokwe na ujinga wake. Anza leo kujijengea ujasiri ili uweze kufikia malengo na Ndoto zako. Kubali kuwa hujui ili uweze kujifunza kwa wengine.

Mafanikio yanawezekana kama ujajitia ujasiri na kuthubutu.

Endelea kujifunza kila siku.

Kubali kwamba wewe ni mjinga maana hakuna anaejua kila kitu. Kuna mengi sana wewe unayajua mimi siyajui na kuna mengi pia ambayo mimi nayajua wewe huyajui tunaweza kusaidiana na tukafikia mafanikio yetu.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading