HATUA YA 298: Uaminifu Huu Umezidi Yote.

Wakati ambao hakuna mtu wa kukufuatilia wala kukupangia cha kufanya ndio tunaweza kujua ufanyaji wako wa kazi ukoje. Ile bidi utakayoionyesha kwenye kazi na hakuna mtu anaekutazama ndio bidi yako halisi.

Vile vile kwenye mambo mengine, kama wewe haupo kwenye mahusiano zile tabia ambazo unakuwa nazo kipindi hicho ndio tabia zako halisi. Kama umekuwa mtu ambaye unasema napenda Maisha ya hivi hakuna wa kuniuliza nimerudi saa ngapi wala nilikuwa wapi, basi jua hizo ndio tabia zako za ukweli.

Kipimo kizuri cha kuujua uaminifu wa mtu sio wakati ule ana kitu cha kumlazimisha awe mwaminifu. Ukitaka kujua kama mtu alikuwa mwaminifu angalia anachokifanya wakati hana jambo linalomlazimisha awe mwaminifu.

Haihitaji kwenda kwa mtu akutabirie zile tabia na Maisha ambayo unayaishi baada ya kuingia kwenye mahusiano kama ni tofauti na yale ambayo upo single maana yake unafanya maigizo.

Pale ambapo hakuna wa kukusukuma wala wa kuitazama simu yako yale unayofanya wakati huo ndio tabia zake za halisi.

Cha Kufanya;

Kamwe usijidanganye jaribu kuishi yale Maisha ambayo wewe mwenyewe hujisikii hatia ndani yako. Bila ya kusukumwa na kuulizwa na yeyote fanya kwa ajili yako na kwa ajili ya kusudi lako.

Kama utashindwa kujijali mwenyewe huwezi kumjali mtu mwingine. Uaminifu kwako mwenyewe ndio wa muhimu kuliko ule unaoonyesha ukiwa na wengine.

Muda mwingi Zaidi upo na wewe mwenye hivyo usiwe unajidanganya. Ishi vile ambavyo ungetaka uje kusimulia kwa watoto wako.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

This entry was posted in HATUA ZA MAFANIKIO and tagged , on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *