Hapo ulipo sasa usipadharau na kujiona upo nyuma sana. Kuna wengi sana wanatamani wafikie HATUA uliyofikia wewe. Kuna wengi wanajifunza kwa HATUA uliyofikia leo.

Hata kama huoni wanaokupongeza kuna watu wanajifunza mno juu ya kile unachokifanya. Ninasema hivi Kwasababu inawezekana umekata tamaa na kujiona uko chini na wakati Mwingine kutokujali kile ulichonacho sasa. Kijali sana na kitunze kile ulicho nacho sasa maana ndio kinakuweka mjini.

Simu uliyonayo sasa ijali na iheshimu maana ndio inakuweka mjini na kukufanya uweze kuwasiliana. Usiidharau Kwasababu umeona wenye nzuri zaidi yako.

Nguo ulizonazo ni za maana sana maana ndio zinakusitiri hadi sasa. Hata kama unaona sio nzuri kama za wengine jaribu kuzikosa sasa hivi.

Biashara uliyonayo haijalishi ni ndogo kiasi gani. Ijali na iheshimu maana bila hiyo inawezekana jana ungelala njaa. Usitamani vikubwa ukasahau kujali vile vidogo vinavyokufanya uishi sasa hivi.

Kazi uliyonayo ni ngumu na ina mateso sawa. Lakini embu jaribu kujiona ukiwa huna hiyo kazi utaishi maisha gani?  Hata kama mshahara ni mdogo embu jione ukiwa huna hata huo mshahara mdogo utaishi vipi?  Embu waangalie wenzako walioko mtaani wanaoitamani kazi yako?

SULUHISHO: Usiidharau ulichonacho sasa maana ndio kinakufanya uweze kuona vingine Vizuri.

Kama ni Biashara jifunze namna ya kuongeza ikue. Kama ni ajira jifunze namna ya kuanzisha Biashara ukiwa ndani ya ajira. Kama ni nguo nzuri jifunze kuweka akiba ununue kidogo kidogo. Kama ni simu nzuri jiulize unaitaka kwa ajili ya status au matumizi yako yamefikia kumiliki simu hiyo?  Kama ni sawa fanya maamuzi.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading