Kama kuna sehemu utakosea ni kusahau kujali vitu vya muhimu sana kwenye Maisha yako wakati unatafuta mafanikio na mali za ulimwengu huu.

MAHUSIANO;
Wakati unatafuta pesa usijisahau ukaacha kutengeneza mahusiano mazuri na familia au wale unaowapenda.
Unaweza kutafuta pesa nyingi sana kwenye dunia hii kisha unashindwa kuja kuzifurahia kwasababu wale unaowapenda na waliokupenda uliwasahau hivyo ukawapoteza.

Unaweza kutafuta mafanikio ukasahau watoto, mke, rafiki na wengineo. Hii ni hatari sana hakikisha familia yako inafurahia uwepo wako. Bila familia sisi sio kitu, bila familia hakuna muunganiko wowote ambao ungetokea. Jali sana familia yako, ndugu zako, marafiki na wote uwapendao.

Kama wako mbali na wewe tenga muda mfupi ambao unaweza kuwakumbuka kwa ujumbe mzuri au hata kuwapigia simu. Tambua kwamba kuna siku watakuwa hawapo tena duniani. Vyote uvitafutavyo haivitakuwa na maana sana kama wale unaowapenda hawapo.

AFYA;
Wakati unatafuta mafanikio kwa nguvu zote usijisahau ukashindwa kuijali afya yako. Afya ndio inakupa uwezo wa wewe kufanya yote hayo unayotaka. Ukisahau afya huwezi kuishi kwa furaha wala kufurahia unachokitafuta.
Siku zote kama una bidi katika kutafuta ongeza bidi katika kujali afya yako. Fanya mazoezi kula vyakula bora. Na hakikisha unaishi kama unavyoweza kuishi sasa.
KUMBUKA: Hakikisha unafanya yote kwa pamoja. Kama unatafuta pesa tafuta kwa bidi sana lakini jail afya, jail wale uwapendao. Kama unatafuta mafanikio tafauta kwa bidi zote lakini usisahau afya yako. Usisahau watu wa muhimu kwenye Maisha yako. Jiulize hivi kwa mfano ukapatwa na janga la kupoteza kila kitu ulichonacho ni wapi utaanza kukimbilia? Huyo alikuja kichwani kwako wa kwanza hakikisha unamjali na kumuonyesha uwepo wako.

Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading