Ukiona mtu anatumia nguvu kubwa kupambana na mtu asiye na nguvu hata nusu yake basi ujue mtu huyu ni dhaifu kuliko yule anaejaribu kupambana nae. Huwezi kushindana na mtu anaeongea kwa kutumia silaha njia pekee ya kuweza kusema wewe umeshindana nae ni kwa kutumia maneno kama yeye.
Najua umewahi kusikia visa vya mtu kumpiga mke wake hadi kumuua au kumuachia majeraha ya Maisha, hii yote inaletwa na watu ambao ni dhaifu kabisa wameshindwa kutumia fikra zao kufanya maamuzi sahihi. Ukiona umefikia kutumia nguvu kwa mtua asiye na nguvu maana yake wewe ndiye ulieshindwa.
Mtu alie imara ni yule anaeweza kudhibiti hisia zake hasa hisia za hasira. Kama mtu akikutukana hupaswi kumjibu kwa matusi wala kwa kupigana nae njia rahisi ya kumjibu ni kumpuuza.
Sasa watu wengi ambao huwa hawapendi kuonekana wameshindwa wanaishia kutumia nguvu kubwa kuonyesha kuwa na wao wanaweza. Ni sawa na mtu anaejaribu kuua mende kwa kutumia nyundo ni kweli utamuua lakini utaonekana huna akili sawa sawa.
Mtu dhaifu kuliko wote sio ambaye hana nguvu bali ni yule anaeshindwa kuziongoza hisia zake na hasira juu ya watu ambao wamemuudhi. Inawezekana mtu huyu akawa ni baba kwenye familia, au kiongozi sehemu Fulani yote ni sawa kama utashindwa kutumia busara maana yake wewe ni dhaifu.
Haijalishi wewe una ujuzi na uwezo mkubwa kiasi gani katika kupigana kama ukienda kutumia nguvu hizo na ujuzi huo kupigana na asiye na ujuzi kabisa wewe ndio unaonekana huna akili timamu.
Kama unafikiri una uwezo mkubwa katafute mwenye uwezo unaoendana na wako ndio mshindane.
Kama utaweza kuziongoza hisia zako vizuri hasa pale mtu anapokuwa amekukasirisha utakuwa ni mshindi kwenye jambo lile. Usikubali kuonyesha udhaifu wako kwa kutumia hisia Zaidi badala ya akili.
Ni mimi Rafiki Yako,
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/