HATUA YA 302: Jinsi Unavyopoteza Nguvu Zako Bila Ya Wewe Kujua.

jacobmushi
3 Min Read

Katika Maisha kuna mambo mengi sana tunafanya kila siku mengine ni kutokana na mazoea yetu na mengine ni yale ambayo tunapanga kufanya. Katika mambo ambayo yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye Maisha yako ni yale ambayo umekuwa na mazoea ya kuyafanya.

Kutokana na mambo ambayo umezoea kuyafanya kuna ambayo yanaweza kuwa na faida kwako na mengine yanaweza kuwa na hasara kwako. Shida kubwa inakuja pale ambapo wewe unafanya tu kwavile imeshakuwa tabia yako hivyo hufikirii tena kwa undani juu yake.

Mfano wewe umejijengea tabia ya kufuatilia tamthilia nzuri kwenye king’amuzi chako, baada ya muda inakuwa ni mazoea yako. Ukirudi nyumbani unakuwa bize kujua pale ulipoishia jana ili uendelee tena leo. Shida inakuja pale kwamba muda wako mwingi unakwenda kwenye vitu kama hivi ambavyo havina matokeo mazuri kwenye baadae yako. Kwa kuangalia tamthilia kila siku kuna matokeo ya wewe kuja kuwa na Maisha magumu huko baadae.

Kwa kujenga mazoea ya kunywa pombe kila siku unajitengenezea tabia ambayo baadae itakuletea umaskini mkubwa.

Kuna vitu vingi sana ambavyo vinatoa pesa mfukoni kwako na havina maana sana kwenye Maisha yako ya baadae hata kidogo. Mtu yupo tayari asipitwe na jambo ambalo akishalifahamu tu linakuwa halina maana tena kuliko akanunua kitabu.

Tunaweza kusema kwamba yale mambo ambayo yanatoa pesa mfukoni kwako na wewe hupati thamani yeyote maana yake ni kwamba nguvu zako, muda wako, pesa zako zimetumika bure. Umepata kiburudisho cha muda mfupi tu na baada ya hapo kesho utahitaji tena.

Ubaya ni kwamba yale mambo mazuri ambayo ungewekeza nguvu zako, muda wako na pesa zako ni magumu sana kwasababu kwa wakati huo unakuwa huoni faida yake. Kwa mfano unapotakiwa usome kitabu na kuangalia Tv, kuangalia Tv ni raha unapata kiburudisho lakini kusoma kitabu inakuwa kama ni kazi ngumu hivi.

Matokeo ya kusoma kitabu, na matokeo ya kuangalia Tv mara kwa mara, yanatofautiana. Ukijenga tabia ya kufuatilia vitu ambavyo vinakuletea raha tu utaishia na mwisho mbaya. Ukijenga mazoea ya kusoma vitabu mara kwa mara mwisho wako utakuwa mzuri hata kama ni miaka 20 ijayo bado kuna faida kubwa.

Fanya kila jambo kwa kiasi na usikubali kuwa mlevi hasa kwenye mambo yasiyo na faida kwenye hatma ya maisha yako.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading