Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.

ZABURI 119:9

Kwa dunia ya sasa ambayo imejaa kila aina ya uovu hasa katika kundi hili la vijana ni muhimu sana kwa kila mmoja kujua ni namna gani anaweza kutengeneza njia ambayo ni safi mbele za Mungu.

Ni kwa kupitia njia safi tunaweza kuyafurahia Maisha yetu hapa duniani.

Kwa kupitia njia iliyo safi tunaweza kuacha alama ambayo ni mfano kwa kizazi kijacho.

Wengi wamefika sehemu kubwa za Maisha yao lakini wanashindwa kueleza namna walivyoweza kufanikiwa kwasababu ya mambo machafu waliyofanya.

Wengi wamefika sehemu ambayo Maisha waliyoishi wanasema hawataki kabisa watoto wao wajue na pia waishi hivyo.

Wewe kama kijana bado una nafasi ya kusafisha njia yako ili uwe na Maisha ya mfano mzuri kwa watoto wako na kwa kizazi kijacho.

Unaweza kuamua kuwa mfano wa kuigwa au mfano wa kutokuigwa.

Unaweza kurekebisaha bila ya kujali ambayo yameshatokea mpaka sasa kwenye Maisha yako. Lile ambalo unataka litokee kwenye Maisha yako bado linaweza kutokea katika njia sahihi na zenye baraka kwenye Maisha ya wengine.

Ni kwa kutii na kulifuata neno la Mungu ndio njia ya kumwezesha kijana kuisafisha njia yake.

Ni vizuri kutenga muda wako na kulitafakari neno la Mungu kila wakati ili uweze kujua anasema kitu gani na wewe kwenye Maisha yako.

Maisha yako yaweke mikononi mwake na umtangulize kwenye kila Hatua unayotaka kuchukua kwenye Maisha yako.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading