HATUA YA 304: Usipoacha Tabia Hii..

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

 

Wakati unaendelea kulalamika na kutoa sababu nyingi za kujitetea kwa hali uliyonayo sasa hivi:

Bado una muda mwingi wa kutumia simu yako kuperuzi kila kinachoendelea mitandaoni.

Bado una muda wa kutazama tamthilia ndefu kwa masaa kadhaa.

Bado una muda wa kukaa sehemu na ukapoteza muda ukiwasema watu na serikali jinsi ambavyo haijakufanyia vizuri.

Bado una muda mwingi wa kupoteza na marafiki wasio na mchango wowote kwenye Maisha yako na Ndoto ulizonazo.

Unachosahau ni kwamba muda wote huo unaopoteza ungeweza kuutumia kwenye kufanya mambo ambayo yangekupatia nafasi ya kutimiza Ndoto yako.

Hilo unaloliona ni lisaa limoja tu umetumia ungeweza kusoma kitabu na kikakupa mwangaza wa kuchukua Hatua Fulani kwenye Maisha yako.

Ungeweza kuutumia muda huo kidogo kufanya jambo ambalo lingekupa nafasi ya kusogea mbele.

Lazima kubali kubadili aina ya Maisha yako uliyokuwa umezoea kuishi. Lazima ukubali kuacha tabia ambazo umekuwa nazo na zimekufikisha hapo.

Kuna nyakati itakubidi ukose usingizi ili uweze kutimiza malengo yako Fulani. Kuna wakati itakubidi ukubali kujiumiza ili upige Hatua Fulani kwenye Maisha yako.

Kaa mbali na vitu vinavyochukua muda wako na hakuna matokeo yeyote ya sasa wala ya baadae yenye mchango chanya kwenye Ndoto yako. Kutumia muda wako kuperuzi mitandaoni na kutazama filamu ni sawa na kula makapi ndani ya mwili wako.

Acha kupoteza muda kufanya yasiyo na maana kwenye Maisha yako. Fahamu kile unachokitaka sasa hivi na ukifanyie kazi kwa namna yeyote ambayo ni halali.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading