Haijalishi unapitia hali gani sasa, unapaswa kujipa moyo na kujitia nguvu kwasababu wakati wa wewe kufanikiwa na kuinuka kwenda viwango vingine upo.

Unaweza kupambana sana na kutumia kila njia ambazo unafundishwa na unazosoma kwenye vitabu lakini ukajishangaa kwamba hakuna mabadiliko yeyote.

Unapaswa kuendelea kujipa moyo kwamba hautabaki kama ulivyo milele. Asubuhi yako inakuja usitishwe wala kukatishwa tamaa na hali uliyonayo sasa.

Inawezekana upo gizani na hakuna dalili yeyote ya mwangaza, napenda nikutie moyo kwamba hutabaki kama ulivyo milele.

Wakati wako upo, endelea kuwa na Imani.

Endelea kuwa na Tumaini.

Mungu anajua na anayaona mapito unayopitia. Kuna mapito unaweza kupitia wewe kumbe ni funzo kwa ajili ya wengine. Endelea kufanya yale yaliyo sahihi na umuachie Mungu yale ambayo hayapo kwenye uwezo wako wa akili.

Usikate tamaa kwa kuwa bado upo hai endelea kutenda wema kila iitwapo leo. Maisha yako Mungu anayajua na anakufahamu kuliko unavyojifahamu wewe. Yeye anajua kila unachokitaka na kule unakotakiwa kwenda.

Wakati mwingine unatakiwa ujifunze kumuachia Mungu yale ambayo sio saizi yako ayashughulikie.

Endelea kuamini kwamba Hutabaki Kama ulivyo siku zote.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading