HATUA YA 307: Huu Ndio Uhuru Wa Kweli.

Uhuru sio kuamua kufanya unachokitaka bila kupangiwa au kusimamiwa na mtu yeyote. Endapo ingekuwa ni hivyo basi kungekuwa na uharibifu mkubwa kwasababu ya asili yetu wanadamu.

Wanadamu tuna asili ya kutokutosheka na pia ukichanganya na wale walio na nia zisiozo nzuri unakuwa unatengeneza uharibifu Zaidi.

Pamoja na kwamba unaweza kuwa na nguvu nyingi sana za kukuwezesha kufanya chochote ukishindwa kudhibiti nguvu hizo zinageuka na kuanza kukutumikisha.

Unaweza kuwa mtumwa wa hisia kama utaziruhusu hisia zikuongoze wewe katika kufanya maamuzi badala ya wewe kuziongoza hisia zako. Mwanzoni unaweza kujiona upo sawa lakini kadiri muda unavyokwenda ndipo utagundua upo kwenye kifungo.

Uhuru wa kweli upo katika kuweza kudhibiti na kuongoza tamaa zako, nguvu zako, mahitaji yako ya kimwili. Uhuru wa kweli sio kufanya unachotaka kufanya tu.

Watu wengi hufikiri wako huru lakini ukichunguza kwa undani unakuta ni watumwa. Unaweza kuwa mtumwa kihisia, hisia zako zikakutumikisha kufanya vitu vya ajabu hadi watu wakashangaa. Wasioelewa watasema kila mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka lakini werevu watajua kwamba wewe ni mtumwa wa hisia zako.

Hakikisha unaweza kujiongoza na kujidhiti, sio kila ambacho unakitaka ni kweli unakitaka.

Jitengenezee utamaduni wa kujiongoza, na wakati mwingine unaweza kujinyima vitu ambavyo sio vya lazima sana kwenye Maisha yako.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *