HATUA YA 308: Maoni ya Watu Wengine Juu Yako.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Tumezungukwa na watu wengi ambao wanatutazama kwenye yale tunayofanya kila siku. Wapo ambao wanatupenda na wanatamani kuona tunafika mbali vilevile wapo ambao wanatuchukia tu na wanatamani siku zote kuona tunateseka.

Ni vyema tu ukaelewa hilo kwamba kuna watu wa aina hiyo kwenye Maisha yako na kile ambacho unakifanya. Ukiweza kutambua hivyo utajua namna bora ya kuchukuliana na watu kwa yale ambayo wanasema juu yako.

Kuna nyakati unaweza kupokea maoni ya kila namna ambayo kwa nje yatakuwa yanaonekana ni mazuri sana kumbe ndani yake yana nia ya kukupoteza. Adam na Hawa walipoambiwa na nyoka kwamba matunda ya mti ule wakiyala watafanana na Mungu ndipo walikubali kuvunja yale maagizo waliyopewa.

Maoni ya shetani yalionekana ni mazuri sana, lakini kumbe ulikuwa ndio mwanzo wa uharibifu mkubwa.

Sio kila maoni na ushauri unaopokea hasa ule wa watu wanaokuja baada ya kuanza kuona unaanza kupata mafanikio ya hapa na pale. Hawa wengi wanakuwa ni sumu wameleta. Wengine pia wanakuja tu kuongea ili wasionekane walikaa kimya.

Ukitaka kujua watu ambao wanafaa kwenda na wewe ni wale ambao ulikuwa nao wakati huna chochote. Wale waliokuwa wanakutia moyo na wakati mwingine hata kukuazima pesa ya kula nyakati zikiwa ngumu.

Kuna watu furaha yao siku zote ni waone upo chini yao. Ukiwa unalia shida hakuna anaeonekana akiongea chochote lakini ukiwa umepandishwa juu kidogo ndipo wanakuja kujifanya wako pamoja na wewe.

Kuwa Makini na Chuja Vizuri Maoni Unayopokea Kwa wengine.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading