HATUA YA 310: Ni Kama Kivuli Tu.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Maisha Yako yaliyokwisha kupita ni kama kivuli nyuma yako. Sio kila mtu anaekutazama ataweza kuona kivuli chako labda awe alishakuwa nyuma yako. Unachotakiwa kujua ni kwamba kivuli hakiwezi kuondoka hasa unapokuwa kwenye mwangaza.

Pamoja na kuwa kivuli chako kinaendelea kukufuata hakitakiwi kiwe sababu ya wewe kushindwa kusonga mbele. Ni kweli kuna vivuli vingine vinatisha sana lakini unatakiwa uendelee kukichukulia kama kivuli tu ambacho hakina nguvu yeyote.

Kivuli kinamtegemea yule aliesababisha kivuli kile kionekane. Wewe ndio unaweza kukiongoza kivuli chako usikubali kivuli chako kiwe mbele yako kiache nyuma wewe songa mbele.

Nimesema Maisha yako ya nyuma ni kama kivuli na yatakufuata popote uendako kwasababu huwezi kuyafuta na kufanya kama hukuwahi kuyaishi. Haijalishi utajitahidi kusahau kiasi gani lakini bado itabakia kwamba ulishawahi kuishi Maisha Fulani.

Usitumie muda wako kutazama kivuli utashindwa kwenda mbele. Jifunze kwamba kivuli chako kikiwa kizuri kitakuwa faraja kwa wale wanaokuja nyuma yako. Kikiwa ni kibaya kinaweza pia kuwa somo kwa wanaokuja nyuma yako pia.

Usikubali kubeba mizigo ndani ya moyo wako kwa kuendelea kuumizwa na yale ambayo yameshapita. Ukubali ukweli kwamba hayo yalikuwa ni Maisha yako lakini sasa una Maisha mengine. Ukubali ukweli kwamba hauwezi kubadili chochote kilichopita bali unaweza kubadili kuanzia leo na kuendelea.

Vile ambavyo unataka Maisha yako yawe unaweza kuanza kutengeneza kuanzia sasa. Achana na vivuli ambavyo vilishapita.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading