HATUA YA 315: Hiki Ndio Kipimo cha Thamani ya Unachokifanya.

jacobmushi
2 Min Read

Lipo swali moja ambalo unapaswa kujiuliza kila wakati kwenye kile ambacho unakifanya kila siku. Inaweza kuwa ni kazi yako, kipaji, biashara au chochote kile kinachokuhusisha wewe na watu. Ni jambo jema sana kujua maendeleo yako na kama kweli unachokifanya kinaongeza thamani kwa wengine.

Lazima ujiulize, Hivi nikiacha leo kufanya hiki kitu Itakuaje?

Kama ni ajira; Bosi wangu atasemaje?

Wafanyakazi wenzangu watasemaje?

Wateja niliokuwa nawahudumia watajisikiaje wasipokuwa wananikuta tena?

Kam ni Kipaji chako au Chochote Kinachogusa Maisha ya wengine;

Hawa watu waliokuwa wananifuatilia wasiposikia tena kutoka kwangu itakuaje?

Je unafikiri kuna kitu watakuwa wamekosa? Unafikiri kuna namna watafanya angalau wajue ulipatwa na nini? (sio muhimu sana) Je kuna pengo utaliacha?

Tukichukulia mfano wa Bongo Movie kuna watu mpaka sasa wanasema Pengo la Marehemu Kanumba halitakaa liweze kuzibika. Hii ni kwasababu aliweza kukitumia vyema kipaji chake na kuwafunika wenzake kabisa. Sasa ni vyema ujiulize wewe pengo lako litazibika?

Kuna watu wakiacha kazi mabosi wao watafurahia sana maana wlaikuwa wanatafuta njia ya kumuondoa lakini wanakosa. Kuna watu wakiacha kile wanachokifanya hakuna atakaejua kama walikuwepo kwasababu hakuna cha tofauti walichokuwa wanafanya.

Ni vyema ujiulize na ufanye tathmini kwenye kazi yako.

Weka viwango ambavyo unavitaka na uvifanyie kazi. Usiridhike kabisa na kile ambacho unakipata au unachokitoa kwa sasa.

Kuwa na maono makubwa,

Kuwa mbunifu kwenye kila jambo lako.

Hakikisha unakuwa wa tofauti ili watu waweze kubaki na wewe.

Tengeneza namna ya kuwafanya watu ambao wanapokea kutoka kwako wawe tegemezi, (kuwe na vitu ambavyo hawavipati sehemu nyingine yeyote)

Tengeneza namna bora ya kujiboresha kila wakati.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading