Ulishawahi kwenda mahali ukapotea njia? Unajua ni faida gani unapata baada ya kupotea njia? Kwanza unakuwa umejua njia nyingine ambayo haiendi kule ulipokuwa unakwenda.

Pili utakuwa umegundua njia ambayo itakufikisha kule ulipokuwa unataka kwenda kwasababu ulipopotea uliuliza kisha ukaelekezwa.

Sasa kama wewe ulikuwa hujui kule ulipokuwa unakwenda na ukaweza kwenda bila ya kupotea kuna hatari moja inakujia. Kwanza kuna siku utakuja kupotea na siku hiyo inaweza kuwa ya muhimu sana kuliko siku nyingine hivyo unaweza kuwa umepoteza vitu vya muhimu Zaidi.

Unapoanza kitu chochote kipya usiogope hata kidogo kukosea kwani unakuwa unajifunza njia nyingi Zaidi ambazo hutazitumia kufanya kile unachokifanya bali unaweza kuzitumia hizo njia kufanyia kitu kingine.

Unapokosea mara nyingi unapata nafasi ya kufanya kitu ambacho ni bora Zaidi kwasababu unakuwa umefanya kwa umakini Zaidi ile njia ya mwisho hadi ukapatia.

Kinachowafanya wengi waogope kukosea ni ile hali ya kushindana na wengine. Unajua mkiwa wawili mnafanya kitu kimoja hakuna ambae atatamani afanye kosa hata dogo ambalo litakuwa sababu ya mwenzake kumpita. Lakini unasahau kwamba unaweza kuwa wa kwanza lakini ukiwa huna uzoefu mzuri na mkubwa kuliko yule ambaye alikosea mara nyingi hadi akashinda.

Chochote unachokifanya usiogope hata kidogo kuanguka, unachotakiwa kuwa nacho makini ni kuangali ni vitu gani hasa umejifunza pale ulipoanguka au ulipoyumba.

Songambele, na usiishie njiani hadi utimize Ndoto yako.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading