Inawezekana wewe ni Mkristo na umekuwa unaikumbuka hii siku kuu ya Pasaka kila mwaka, lakini lipo swali la muhimu kujiuliza. Je tunajifunza nini? Pia haijalishi wewe ni dini nyingine yeyote au pia huamini kama kuna Mungu, bado unapaswa kuangalia katika namna ya kujifunza.

Lipo jambo moja kubwa ambalo kila mmoja wetu anaweza kulipata kwenye siku kuu hii ya Pasaka. Ni muhimu sana tukajua tumekuja duniani kuishi na katika kuishi vizuri ni pale unapoweza kuyaishi Maisha yako kwa ajili ya wengine. Sio lazima uutoe uhai wako ndio uwe umejitoa kwa ajili ya wengine  kama alivyofanya Yesu.

Ipo nafasi ya wewe kuishi kwa ajili ya  wengine kila siku, kwa kupitia vile vitu ambavyo Mungu ameweka ndani yako. Una vipaji vizuri ndani yako, vitumie kwa ajili ya wengine. Nafasi ya kazi uliyopata sio kwa ajili yako tu. Kuna wengi nyuma yako ambao wanakutegemea uitumie vizuri nafasi hiyo. Wapo wale ambao unawahudumia kila siku, ipo familia yako inategemea ufanye kazi vizuri ili wawe na Maisha bora.

Kwa vyovyote vile ili ufanikiwe ni lazima ujifunze kuishi kwa ajili ya wengine. Ukiwa mbinafsi utaishia kuwa wa kawaida na wakati mwingine kujitengenezea matatizo. Uwezo ambao umepewa sio kwa ajili yako, ni lazima wengine wafaidike kwanza ndipo na wewe uanze kuona matunda yake kwenye Maisha yako.

Jifunze kuwatumikia wengine kwa nafasi uliyonayo kwenye jamii.

Ili uweze kuwa mtu wa watu lazima ujifunze kujitoa kwa ajili ya wengine.

Ziweke zile faida unazotaka kupata pembeni na weka nguvu nyingi kwenye kuwahudumia watu.

Watu wengi wanakwama kwasababu huweka matakwa binafsi mbele yao kuliko kuwahudumia wengine. Unapoweka wengine mbele yako huwezi kuchoka kufanya kile unachokifanya na mafanikio yatafunguka mbele yako.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading