Offa, Ya Vitabu Bora Mwezi April. https://jacobmushi.com/offa-offa-offa-ya-vitabu-bora-mwezi-april/
“Because a thing seems difficult for you, do not think it impossible for anyone to accomplish.”
― Marcus Aurelius
Kwasababu kitu kimeonekana ni kigumu kwako, usifikiri haiwezekani kufakiwa kwa wengine pia. Kuna tabia ya wengi kupenda kutoa mfano wa walio shindwa jambo ambalo wameona unataka kufanya. Pia mtu mwingine anaweza kuja akakwambia wewe nilishajaribu nimeshindwa utakuwa unapoteza muda.
Kwanza nipende kukwambia usikubali kuwakatisha tamaa wengine kwasababu tu wewe ulishindwa. Kila mtu ana uwezo wake wa tofauti. Kila mtu kuna jambo ambalo ameandikiwa atafanikiwa kwa hilo, sasa kama wewe ulikwama usiwakatishe tamaa wengine.
Unajua hata kwenye mahusiano wewe unaweza kuwa na mtu mkashindwana kabisa lakini baada ya kuachana mwenzako akapata mtu ambaye wakawezana na kufurahiana sana. Sasa wewe ukibaki unasema yule hafai, ana tabia hizi na hizi, unakuwa unapoteza nguvu zako bure. Hukupangiwa kuwa nae ndio maana mlishindwana. Ni ngumu kulazimisha hatma ambayo haikuwepo lazima kila mmoja atajikuta anakwenda kule alipopangiwa.
Ukweli ndio huo kama ulishindwa wewe kubali kwamba ni wewe ndio ulishindwa lakini bado wengi watafanya na watafanikiwa. Wengi watakuja wataweza kufika sehemu ya mbali Zaidi yako.
Pale alipoishia baba yako sio sehemu ambayo unatakiwa uishie wewe pia. Alipoishia baba yako ndipo unatakiwa uanzie. Hata kama alishindwa haina maana na wewe utashindwa. Kila mmoja ana uwezo wa kipekee ndani yake kwa ajili ya kufanikiwa.
Watie moyo wote wanaotaka kufanya kile ambacho umeshakifanya bila ya kujali umefanikiwa au uliefeli. Umeingia kwenye ndoa ikawa ndoano usiwakatishe tamaa wengine. Kama hukujipanga wewe, waambie tu wajipange ila usiwaambie kwamba ndoa ni mbaya. Usiwatishe watu kwasababu wewe ulishindwa inawezekana ni upungufu wa mawazo uliokuwa nao.
Offa, Ya Vitabu Bora Mwezi April.
https://jacobmushi.com/offa-offa-offa-ya-vitabu-bora-mwezi-april/
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”