Bonyeza hapa upate offa ya Vitabu Bora Mwezi April. https://jacobmushi.com/offa-offa-offa-ya-vitabu-bora-mwezi-april/

Miaka michache iliyopita katika nchi moja hapa barani Africa kulikuwa na baba mmoja ambaye alikuwa maarufu sana kwa kuuza supu sana pembezoni mwa barabara. Baba huyu hakusoma shule hivyo alikuwa hawezi kusoma magazeti. Masikio yake yalikuwa na matatizo kidogo hivyo hakuweza kusikiliza redio wala taarifa za habari zilizokuwa kwenye redio. Kwasababu ya uzee wake macho yake pia yalianza kupata shida hivyo hakuweza pia kuangalia Tv. Vile vile kwasababu ya ubize kwenye biashara ya supu hakupata muda wa kukaa na wazee wenzake wapige stori za hapa na pale.

Siku moja mtoto wake wa pekee aliekuwa anasoma chou kikuu alikuja likizo nyumbani. Alipofika nyumbani wakawa katika maongezi na baba yake. Mtoto akamwambia baba, “Hivi hujasikia hali mbaya iliyopo hapa nchini?, watu wanafunga biashara zao kila mahali, yaani vyuma vimekaza kila sehemu” tunapaswa kujiandaa kwa hali mbaya ambayo inaweza kutukuta hata sisi.

Baba akajisemea moyoni, haya asemayo mwanangu ni kweli, kwanza mimi sijaenda shule, wala sifuatilii habari. Yeye ni msomi atakuwa anajua mambo mengi kuliko mimi, wacha nimsikilize tu. Kesho yake alipokwenda kazini kwake wakati anachukua oda ya supu akapunguza kiasi alichokuwa anachukua kila siku.

Alipofika kazini ile hamasa ya kuuza kama mwanzo ikawa imepungua. Hofu na mawazo ya hali mbaya itakayokuja aliyoambiwa na mwanawe ikamfanya ashindwe kuuza kama zamani. Baada ya wiki kama tatu hivi mauzo yalishuka sana, wateja wakaanza kupungua kwa kasi. Akawa anabakiza supu kila siku.

Akarudi nyumbani na kumweleze mwanae, “mwanangu ulisema kweli, hali mbaya imeshafika hadi kazini hakuna tena wateja. Ni bora uliniambia mapema nikajiandaa na kuweka akiba”

Unatumia Mtandao wa Instagram? Bonyeza mandishi haya unifuate (follow) www.instagram.com/jacobmushi

Tukiangalia huu mfano unatuonyesha kwamba kwenye Maisha kuna mambo mengi tunayasikia tunayabeba kama yalivyo bila ya kufikiri. Kuna mengi ukiyasikia yanasemwa sio uhalisia uliopo mengi yameongezewa chumvi.

Kuna mengi ukiyasikia yatakufanya uanze kukosa hamasa  kwenye biashara yako, badala ya kuwaza utumie njia gani uuze Zaidi, utabakia unawaza hali mbaya itakayokuja. Badala ya kutuliza mawazo kwenye biashara utajawa na hofu kubwa ya mambo mabaya yatakayotokea.

Nasema hivi kwasababu kuna mengi yanaendelea yana ukweli kidogo sana lakini namna ambavyo yanaelezewa yanakuwa yamejazwa chumvi kiasi ambacho kinamfanya mtu aone kama vile dunia inakwisha kesho. Ni vizuri ukajua kwamba hata kama hali mbaya inakuja isiwe sababu ya kukuondolea hamasa ya kuendelea kufanya kazi kwa bidi. Usiache kile unachokifanya kama kwasababu ya maneno ya kusikia.

Kuna matatizo mengine tunayetengeneza wenyewe, mfano baba huyu alipopunguza kiasi cha nyama aliyokuwa ananunua, hii ilisababisha wateja wengine waje wakute hakuna supu. Kwahiyo ni vyema ukajifunza namna ya kuchuja kile unachokisikia na kuangalia ukweli uko wapi, bila kujalisha aliesema ni nani.

Watabiri wa hali ya hewa wanaweza kutabiri kuna mvua zitanyesha kubwa kesho, hii isikufanye uahirishe kwenda kazini kesho bali jiandae kwa kununua mwamvuli. Mvua ikinyesha utajifunika, isiponyesha mwamvuli utabaki, na wewe utakuwa kazini.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading