Katika Maisha haya tunayoishi mara moja tu! Hapa duniani, ni lazima ujue ni kitu gani gani upo tayari kukifanya hadi siku ya mwisho.
Hata ije mvua liwake jua, ije changamoto ya aina yeyote ile haitakufanya wewe ubadili mawazo yako juu ya kitu hicho.

If a man has not discovered something that he will die for, he isn’t fit to live.” – Martin Luther King, Jr. 

Mwanamapinduzi huko nchini Marekani Martin Luther King Jr alisema kama mtu hajagundua ni kitu gani atakifia huyo bado hajawa kamili katika kuishi.

Jew ewe umeshajua ni Kitu gani utakifanya hadi mwisho? Kitu gani Upo tayari kukipigania kuliko kingine chochote?

Hapa duniani nikwambie ukweli yapo mambo mengi sana ya kufanya. Ukikaa chini ukaanza kuangalia ni kitu gani cha kufanya utakutana na vingi mno. Je wewe umeamua kipi kufanya mpaka unakufa?

Ukitambua ni kitu gani utakifanya hadi unaondoka hapa duniani ndio utakuwa umeanza sasa safari kamili ya Maisha yako.

Usikubali kugusa gusa kila kichokuja mbele yako. Umekutana na fursa ifanye kweli hadi watu waseme hii kitu alifanya mtu Fulani vizuri sana. Kama ni kipaji kitumie sawasawa kuliko mtu mwingine yeyote huku duniani.

MUHIMU: Kama bado hujagundua ni kitu gani upo tayari kukifia utakosa vipaumbele vya Maisha yako. Kila kizuri unachokiona mbele yako utatamani kukifanya. Kila unachosikia kinalipa kitakuvutia ufanye. Mwisho wa siku utaondoka duniani ukiwa hujafanya chochote cha maana. Ndugu yangu usikubali kabisa kuishi Maisha ya aina hiyo. Maisha yakuendeshwa na vipaumbele vya watu wengine. Tengeneza Maisha yako. Acha alama duniani.
Karibu sana.
Usiache kushare na wenzako.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255654726668/+255755192418

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading