Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Mti unajulikana kwa matunda yake. Aina ya matunda ambayo mti unatoa ndio tunasema huu ni mti Fulani. Tabia za mtu ndio hatma ya Maisha yake, vile vitu ambavyo unavifanya kila siku ndio vinaonyesha unakoelekea.

Kama unadhulumu watu mwisho wako ni mbaya sana, utakuja kudhulumiwa na kupoteza kila ulichonacho.

Wewe ni mzinzi utaishia kupatwa na magonjwa ya zinaa, au mfarakano kwenye ndoa yako au Maisha yako kwa ujumla.

Wewe ni mlevi, utaishia kuwa maskini maana pesa zako, nguvu zako, unapotezea kwenye pombe.

Wewe unaiba na kutapeli watu, mwisho wako ni mbaya na wa aibu sana.

Haijalishi unachokifanya unakifanyia gizani au hadharani, matokeo ya matendo yako yatakuja kuonekana siku moja.

Ukitenda mema utapata matokeo ya mema yako.

Unajua ni kwanini sasa wengi wanafanya mambo mabaya badala ya mema wakati wanajua fika matokeo ya kile wanachokifanya?

Mwanzo wa mambo mabaya siku zote ni mtamu na mrahisi, mwisho wake ndio mgumu, mbaya na wenye aibu sana.

Mambo mazuri mwanzo wake ni mgumu sana, unaonekana unafanya mambo ya ajabu na yasiyoeleweka. Lakini baadae watu ndio wanakuja kukuelewa.

Njia rahisi ya kuweza kutabiri mwisho wako au mwisho wa mtu, ni kwa kuangalia kile ambacho mtu anakifanya kila siku. Kile ndio kinaonyesha kule anapoelekea. Kinaonyesha matokeo ambayo atayapata baadae.

Wewe umechagua nini? Kupoteza muda? Kulalamika? Au kufanya kazi?

Acahana na matendo ambayo unajua fika haya yataniletea umaskini, unajua kabisa haya mwisho wake ni mbaya halafu bado unaendelea kushikilia.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading