Kama kila kiumbe hai kitaweza kufuata vile kilivyotakiwa kuishi kila kiumbe kitatosheka. Mwanadamu ndie kiumbe ambaye anaongoza kwa kutokutosheka hapa duniani.  Kutokutosheka ni kile kitendo cha mtu kuacha kutazama vile ambavyo tayari amebarikiwa na kuangalia Zaidi vile ambavyo yeye hana ila wengine wanavyo.

Usiache kutembelea Hapa Ujipatie Vitabu Bora vya Mafanikio na Biashara https://jacobmushi.com/patavitabu/

Kama umewahi kukaa na watoto wadogo unaweza kukuta umeona mtoto mmoja yeye akiona wenzie wana mdoli mzuri au wa tofauti tu na wake ataanza kuulilia. Ukweli anasahau kwamba hata yeye ana mdoli tena unaweza kuwa mzuri kuliko wa wengine wote.

Hii tabia ipo hata tukiwa watu wazima. Ndio maana unaweza kuona mtu anakutakia mabaya tu ili mkose wote. Ndio maana unakuta ukianzisha biashara Fulani nzuri kila mmoja atataka aige ili awe na kama yako.

“Every living organism is fulfilled when it follows the right path for its own nature.”
― Marcus AureliusMeditations

Mwanafalsafa Marcus anatuambia kwamba, “ kila kiumbe hai kinaweza kutosheka endapo kifatuata njia yake kutokana na asili ya kuumbwa kwake”

Yaani kama wewe ni samaki ukitaka kutosheka achana na kutamani kuruka juu kama ndege. Wewe umepewa uwezo wa kuogelea utumie huo. Wewe mwanadamu ukitaka kuishi na furaha achana na vitu ambavyo huna uwezo navyo fanya vile ambavyo ulizaliwa kuja kufanya. Ukisema ukaimbe mziki kwasababu tu Diamond amefanikiwa utapotea.

Chochote unachokifanya hakikisha kimeletwa na msukumo kutoka ndani yako ndio utaweza kukifurahia na pia kudumu katika hicho. Achana na vitu ambavyo vinaletwa na msukumo wa nje hutafika mbali. Watu wanaweza kukuhamasisha kwa yale mambo makubwa waliyofanya lakini haitakiwi uanze kuwaiga wao. Tumia hamasa hiyo kutimiza kile kilichopo ndani yako.

Vitu vitu vya kuiga lakini huwezi kuiga mafanikio ya wengine. Unaweza kuiga mbinu, ujuzi na tabia walizotumia kujenga nidhamu hadi wakafanikiwa lakini sio kuiga kuwa wao.

Usiwe kama mtoto mdogo ambaye anataka yeye ndio apate kila kitu. Anza kutumia kile kilichopo ndani yako hadi kikue. Mengine yatakuja yenyewe baada ya wewe kusogea mbele.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading